06/05/2026
Ugonjwa mbaya zaidi unaokuibia pesa mtandaoni leo hauitwi uvivu. Unaitwa "Laana ya Ujuzi" (The Curse of Knowledge).
Hii ndiyo hali inayokufanya uone kile unachokifanya kwa urahisi kuwa ni kitu cha kawaida ambacho "kila mtu anakijua".
Unadhani kwa sababu wewe unatumia dakika mbili kukifanya, basi hakina thamani.
Unajidanganya. Na huu uongo unakuzuia kutengeneza pesa.
Ngoja nikupe mfano kuntu utakaokufikirisha sana:
Fikiria wewe ni mtaalamu wa kutumia WhatsApp Business. Unajua jinsi ya kuweka 'Auto-reply' na kupanga wateja kwa 'Labels' za rangi tofauti ndani ya dakika tatu tu.
Kwako, hili ni jambo jepesi mno.
Hata ukiamshwa usingizini unaweza kulifanya. Hukumbuki hata ulilijifunzia wapi.
Ukishauriwa utengeneze muongozo wa kufundisha hili, unacheka na kusema, "Nani atanunua kitu rahisi hivi?"
Sasa, mfikirie Mfanyabiashara wa nguo mtandaoni. Anapokea meseji 300 kwa siku. Anashindwa kujibu wote kwa wakati.
Wateja wanamtukana, anapoteza mauzo ya mamilioni, na hapati muda wa kupumzika. Yupo kwenye msongo wa mawazo uliokithiri.
Siku ukimwonyesha ile "mbinu yako rahisi ya dakika tatu", atakuona k**a mchawi aliyeshushwa kumuokoa. Atasema, "Kumbe inafanyika hivi? Mungu akubariki sana!"
Kile unachokiona k**a "ujuzi mdogo usiokuwa na thamani", kwa mtu mwingine ni suluhisho la tatizo linalomnyima usingizi.
Watu hawajui unachokijua. Wanaweza kuwa na akili sana kwenye mambo yao mengine, lakini kwenye hilo eneo lako—wewe ndiye bosi wao. Wanakuhitaji.
Kuna mtu huko nje yuko tayari kukulipa leo ili apate hiyo "njia ya mkato" yako. Acha kuficha ujuzi wako ukidhani kila mtu anajua. Kila mtu HAJUI.
Kile unachokidharau leo ndicho kinachoweza kuwa bidhaa yako ya kwanza ya kidijitali inayoingiza mauzo.
Acha kujidharau.
Tengeneza muongozo wako, upandishe Kinu leo, na uruhusu Affiliates makini wakutafutie wateja wanaohitaji msaada wako.