Pansens +255768 089 616

Pansens +255768 089 616 Friends Forever_

14/07/2024
💥💥💥.studio._ mwanza
26/06/2024

💥💥💥.studio._ mwanza

movements💥💥
24/06/2024

movements💥💥

mwanza tanzania🏖️
20/06/2024

mwanza tanzania🏖️

09/11/2022
09/11/2022

Happy

"M Y W I F E , I A M S O R R Y"Asubuhi aliamka na kumkuta mkewe akisali. Akamsikia mkewe akimuombea. Akamtazama kwa seku...
29/08/2017

"M Y W I F E , I A M S O R R Y"

Asubuhi aliamka na kumkuta mkewe akisali. Akamsikia mkewe akimuombea. Akamtazama kwa sekunde kadhaa. Ni muda mrefu sana tokea amemshuhudia mkewe akisali.

Wamekuwa na ugomvi na kutoelewana katika ndoa yao Kwa miezi kadhaa sasa. Usiku wa jana yake wamegombana ugomvi mkubwa mno.

Haraka haraka Mume akainuka kitandani na kuelejea jikoni kuandaa kifungua kinywa. Kwa hio miezi kadhaa ya ugomvi mkewe amekua hamuandalii chakula. Kwa mshangao, akakuta staftahi imeshaandaliwa mezani. Akala.

Baada ya kumaliza akarudi chumbani, kujiandaa aingie bafuni. Mke nae akawa anatoka bafuni. "Habari za asubuhi. Uwe na siku njema". Mke akamsalimia mumewe na kumtakia kazi njema, huku wakipishana bafuni

Baada ya kuoga, na kuvaa tayari kwenda kazini; akamuona mkewe jikoni, akila staftahi akiwa na amani. Alikuwa akila kifungua kinywa huku akicheka kutokana na kuangalia video za vichekesho alizotumiwa WatsApp.

Mume akamtizama kwa dakika kadhaa halafu, akaelekea mlango wa kutokea na kuelekea kazini. Ule mwonekano wa mwisho aliouona kwa mkewe ukamsumbua nafsi.

Akajisemea nafsini mwake.."hivi sivyo inavyotakiwa awe. Hivi sivyo ambavyo amekuwa siku zote." Mume Amekuwa akimuumiza mkewe, na mkewe hivi karibuni amegundua kwamba mumewe anayo nyumba ndogo, na haitoshi amegundua pia anatembea na wanawake wengi.

Amekuwa akitapanya fedha za familia kwa wanawake. Mkewe lazima awe na hasira dhidi yake. Lakini ile amani aliyomuona nayo mkewe asubuhi ile ilimshangaza na kumfanya ajiulize maswali mengi.

Jioni ikafika. Akarudi nyumbani na kukutana na mkewe aliye na amani tele tena. Alikuwa jikoni akipika chakula cha usiku huku akicheka na wanae. Mke alirudi kutoka kazini k**a masaa mawili yaliyopita.

Wakala. Chakula kilikua kitamu. Chakula kizuri, mke akawa na maongezi ya furaha na watoto wake baada ya kumaliza kula. Yeye k**a baba alikuwa ametengwa kwenye yale maongezi.

Mkewe na watoto wake walionekana kufurahia yale maongezi ingawa baba yao alikuwa akiwaumiza kwa ugomvi na mama yao.

Akiwa anaosha vyombo Baada ya Dinner, huku watoto tayari wakiwa wameshaenda kulala, mume wake akamkaribia. "Uko sawa?" Mume akamuuliza mkewe. "Niko zaidi ya sawa. Nimebarikiwa". Mke akamjibu mumewe huku akitabasamu..

"Umenikasirikia kwa haya nayoyafanya na ambayo nimekufanyia?" Mume akamuuliza tena mkewe.

Mke akaweka kwenye dishi sahani aliyokua anaiosha na kumtazama mumewe. Kisha akaanza kuongea..

"Nilijiuliza nafsi yangu, ni mahusiano gani muhimu katika maisha yangu? Mahusiano niliyonayo na wewe au niliyonayo na Mungu wangu? Na nikagundua mahusiano muhimu kwangu ni yale niliyonayo na Mungu wangu. Naishi kwa ajili ya Mungu. Sio kwa ajili yako...

"Kuolewa na wewe ilikuwa ni baraka lakini si kwamba ndio kila kitu katika maisha. Mungu amenibariki kwa kunipa zawadi ya uhai, sitapoteza uhai wangu kwa kulia kila siku na kuugua vidonda vya tumbo kwa maumivu unayoyasababisha wewe.

Akageukia dishi la vyombo, akachukua bilauri na kuanza kuiosha huku akiendelea kuongea..

"Nimetambua kwamba nilikupa nguvu na uhuru mwingi mno...ndio wewe ni mume wangu, binadamu wa karibu kabisa maishani mwangu na binadamu ninaekupenda sana; lakini wewe sio Mungu. Wewe umefeli lakini Mungu hawezi kufeli na kamwe hawezi kufeli juu yangu..

"Sitaruhusu wewe uniharibie furaha, amani, na maendeleo ambayo Mungu wangu amenipa. Wewe vunja ndoa k**a ndio lengo lako, lakini mimi nitaendelea kumtumainia Mungu wangu..na nitakapoendelea kumtumainia Mungu wangu nitazidi kuwa na furaha licha ya kile ambacho utakua umenifanyia.."

Akaisuza vizuri bilauri na kuiweka katika chombo kisafi...kisha akachukua sahani na kuanza kuiosha huku akiendelea kuongea...

"Ulivokua unaniumiza na kunishushia heshima nilikuwa mwanamke nisie na Mungu. Nilikuwa na hasira na kuharakisha matusi, nilikuwa nataka kulipiza kisasi na nilikuruhusu uendelee tu na ufedhuli wako ili na mimi nianze...

"Performance yangu kazini ilishuka, nikawa siongei na wanangu kwa hasira, nikawa mchungu na mkali kwa watoto wangu, nikapata vidonda vya tumbo...ila hatimae nikagundua yupo Mungu, sitakiwi niwe k**a mtu ambae hana Mungu..kwanini nisiwe na matumaini wakati Mungu yupo?..

"Nilikuwa nime-focus sana kwako kiasi ya kwamba nikamsahau Mungu. Uliponipata, ulinikuta nikiwa na Mungu. Tukaingia katika mahusiano na hatimae ndoa, nikakuachia kila kitu wewe kwa sababu nilitaka ndoa yangu iwe imara...

"Ndoa yetu ikawa nzuri hapo mwanzoni, ndoa yetu imefeli kwa sababu yako wewe kwa sababu uhusiano wangu na Mungu wangu upo palepale..

Akaisuza vizuri sahani, kisha akamgeukia mumewe..akamtazama na kuendelea kuongea..

"Umechagua kuitelekeza ndoa yetu na kunipa mimi kisogo ila hiyo haimaanishi dunia ndio imenigeukia. Nitaendelea kuwa mama bora kwa watoto wetu. Kamwe hutawasikia wakitamka ugomvi wangu na wako ili nionekane mama niliyefeli..

"Wewe endelea kutembea na hao wanawake zako, mimi nitawalea wanangu...

Akakunja mikono yake kifuani, kisha akaendelea kuongea...

"Je ninakuchukia? Hapana, huo utakuwa uongo kusema nakuchukia. Wewe ni mwanaume niliekubali unioe, ambae niliweka agano mbele za Mungu, ambae nakupenda...

Machozi yakaanza kumtoka....akainua mikono yake kujifuta kisha akaendelea kuongea...

"Siwezi kufuta miaka yote ambayo tumekua pamoja. Biblia hata Quran zinatusisitizia kuwapenda maadui zetu. Ikiwa ninao uwezo wa kuwapenda adui zangu, basi ni rahisi sana kukupenda wewe licha ya mabaya ambayo umenifanyia na unaendelea kunifanyia...

"Ndio ninayo hasira na nilikata tamaa, lakini nimeinuka upya. Naishi kwa ajili ya Mungu ambae amenibariki kwa mengi, sio kwa ajili yako na maumivu unayonipa...

Akageukia vyombo na kuendelea kuosha...kimya kidogo kikapita huku mumewe akiwa ameinamisha kichwa chini.

Mke akavunja ukimya uliokuwa umetawala kwa muda kidogo na kuendelea kuongea...

"Kwa ajili ya amani na kukupa uhuru, nafanya mpango wa sehemu ambayo mimi na watoto tutaenda kuishi. Kwa kuwa umeamua kuwa na nyumba ndogo, uliyoipangia na nyumba kabisa, imeonesha kabisa sisi hautuhitaji...

"Hivyo hatutafanya maisha yako yawe ya wasiwasi na kutokuwa comfortable kwa kuendelea kukulazimisha kuishi na sisi...unatakiwa uwe huru kumleta huyo mchepuko wako ndani ya nyumba yako mwenyewe wala sio kumpangia nyumba...

"Nilikuja kwa amani ndani ya hii nyumba, na nitaondoka kwa amani. Hautaua tabasamu na furaha yangu...Mungu wangu hataniangusha katika hili..."

Mke ak**aliza na akaelekea chumbani. Mume akabaki pale k**a nusu saa akitafakari na baadae mume akamfuata mkewe chumbani. Akamkuta mkewe akiwa amelala kwa amani zote. Akamtikisa na kumuamsha. Mkewe akaamka..

"Nakusikiliza...ongea tu" mke akamwambia mumewe...

"Tafadhali sana mke wangu, msiondoke! Sitakuumiza tena, sitakusaliti tena. Kusema kweli mimi siko sawa kabisa. Nahitaji hiyo amani uliyonayo. Nahitaji kuwa aina ya mume k**a wewe ulivyo aina ya mke..ili tuweze kuendana...

"Nimejikuta naumia zaidi kukutenda mabaya, lakini wewe ukiwa bado na amani na furaha tele..hicho kitu kinaniumiza ndani kwa ndani. Namimi nimeamua kurudi kwako...nipokee tena mpenzi wangu..."

Kuanzia siku hiyo, mume akaanza kubadilika huku mkewe akimsaidia kubadilika..hakukuwa na michepuko, hakukuwa na ugomvi, wala kumuumiza tena mkewe...

Mkewe na wanae hawakuondoka. Mume akajinyenyekeza kwa Mungu na akajifunza kuwa mume na baba bora.

Upendo una nguvu kubwa kiasi ya kupunguza kila aina ya ufedhuli.
_____________________________

Sijajua bado ni suala gani gumu unalolipitia mpaka asubuhi hii..ni maombi yangu kwako Mungu akuvushe katika kila aina ya gumu unalopitia..na tazama mvua ya amani itaenda kukunyeshea ikileta uhuru na kumwagilia mbegu ya baraka katika maisha yako.
..AMEN...

Qpans Qp STORYKulikuwa na mzee mmoja ambaye alikuwa tajiri sana, Mzee huyu alibahatika kuwa na binti mmoja na ambaye ali...
23/06/2017

Qpans Qp STORY
Kulikuwa na mzee mmoja ambaye alikuwa tajiri sana, Mzee huyu alibahatika kuwa na binti mmoja na ambaye alimpenda sana na hata
kumwandika kuwa mrithi wa mali zake zote pindi mzee atakapoiaga dunia.

Mzee huyu alimiliki biashara kubwa sana sana na zenye kuingiza kipato kikubwa na aliogopeka
sana sana katika eneo hilo hasa kwa kwa utajiri wake na ukatili wake pia.

Siku moja mzee huyo alipata taarifa kuwa mtoto wake wa pekee alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na kijana mmoja ambaye anatoka
katika familia isiyojiweza na tena ya kimaskini sana,na wazai wake walikuwa wakifanya kazi katika
moja ya mashamba ya tajiri huyo.

Yule tajiri alijawa na hasira na kuona k**a ilikuwa ni fedhea kubwa sana kwa familia yake
na akamuita binti yake na alipomuuliza binti yake alikubalia, mzee kwa hasira akawafukuza
wale wazee na kuahidi kutoa fedha nono kwa polisi yeyote atakaye mtia mbaroni kijana Yule.

Basi kijana Yule ikabidi amfuate binti na kumwambia hali halisi na kuwa sasa wazazi wake wako katika hali mbaya na yeye anasakwa hivyo
ni vyema wakiachana maana anaona Maisha yake yapo hatarini pamoja na familia yake.

Binti Yule akawa akiiba fedha na kuwapelekea wazee wale ili wajikimu na baadae akamshauri
Yule kijana kuwa wakimbie waende mbali wakajifiche na kuanza maisha yao wakiwa k**a mme na mke.

Baada ya mabishano ya siku
kadhaa Yule kijana akakubali na binti akachukua fedha nyingi za kuweza kuanza maisha popote
pale watakapoamua kuishi.

Yule tajiri alipatwa na butwaa na hakuamini k**a binti yake kakimbia, akaamua kuwachukua
wazazi wa yule kijana na kuwafunga bila mafanikio na kuamua kuwaachia huru.

Mkewe na yule tajiri aliendelee kuhuzunika na kunung’unika kwa muda wote mpaka mmewe
akaamua kutoa tangazo kwenye magazeti ya nchi ile na kusema amemsamehe mwanae hivyo
arudi tu na ameafikiana nao kuwa waoane. Hivyo warudi kwa ajili ya harusi.

Taarifa zikamfikia yule kijana akiwa na mpenzi wake yule mtoto wa tajiri, kwa pamoja wakaamua kurudi na wakapokelewa na yule
mzee ambaye akawaambia kuwa watafunga harusi mapema wiki itakayofuata na gharama
zote zitakuwa zake na yule kijana
atashirikiana na yule binti katika kusimamia mali za yule mzee.

Siku tatu baadae wakaamua waende kuandaa suti na shela kwa ajili ya harusi, waingia kwenye
duka la nguo za harusi binti alivyaa shela ikawa imemkaa safi sana na yule kijana naye suti ilimfaya aonekanye maridadi sana,akaamua
kabla ya kuvua ile nguo avuko barabara aende akanunue ice cream maana binti Yule alikuwa
anapenda sana kula ice cream.

Wakati kanunua ile ice cream na anavuka barabara gari likamgonga yule kijana na yule binti baada ya kuona vile alimkimbilia na
alipofika pale damu iliruka na kutengeneza doa kwenye ile shela, wakamchukua na kwenda nyumbani ambako baadae mazishi yalifanyika.

Baada ya mazishi binti Yule aliendelea kuhuzunika na hakutoka ndani kabisa.

Siku moja baada ya miezi kadhaa kupita usiku akiwa kalala alimtokea bibi mmoja na kumwambia katika ile shela kuna doa hivyo
anatakiwa alifuo litoke au balaa litamtokea.

Yule binti kweli asubuhi aliamka na kwenda kuitazama ile shela na kukuta ina doa, akafua sana mpaka doa akaona limeoptea. Lakini
alipolala tena Yule bibi akamtokea tena na kumwambia lile doa halijatakata hivyo afue tena
au balaa itaikumba familia yake.

Siku ya pili akaamka na kufua lakini kila alipofua yule bibi alimtokea na kumwambia vile viele,yule
binti akaona sasa kachoka ni vyema amshirikishe mama yake.

Mama yake akashangaa sana kwani
naye aliota ndoto k**a ile ile na alikumwa akiogopa kuwashirikisha. Mama na mtoto wakanya siri na kulifua tena lile shela na hata
baada ya kulifua yule bibi aliwatokea tena na kuwaambia kuwa bado doa lipo.

Mmmh kazi ikawa ngumu ikabidi wamshirikishe baba, baba naye kumbe wamekuwa akitokewa na
yule bibi na akawa anona sio vyema kuwashirikisha wanafamilia.

Basi baba akawaamuru waichukue ile shelana kwenda kuifukia.

Baada ya kuifukia Yule bibi aliwatokea na kipindi hiki alikuwa mkali zaidi na kuwaambia wana siku mbili tuu za kulifukua lile shela na kulifua mpaka doa litakate la sivyo kuna jambo kubwa litawatokea .

Familia nzima walilifua kwa ushirikiano na wakakubaliana kuwa sasa limetakata na wakalianika na kulipiga pasi baada ya kukauka na uliweka sandukuni.
Usiku wakiwa wamelala.waliambia wameshindwa.

Basi familia siku ya pili walikutana na kusimuliana wote wakaonyesha
kuota ndoto sawa. Siku ya pili wote wakaenda kazini na kumwacha yule binti aiwa nyumbani peke yake.

Akiwa kaka peke yake na huku akisubiri mwisho wake huku akilia kwa uchungu na kumkumbuka
mchumba wake yule kijana,mara mlango ukagongwa na baada ya kumkaribisha binti yule alistaajabu kuona ni yule yule bibi mzee ambaye amekuwa akiwatokea usiku. Lakini mara hii alikuwa kashika kopo dogo mkononi na
kumpa yule binti kasha akaondoka zake.

Je unafikiri Yule bibi kizee alimpa kopo la nini?

Jibu ni kuwa alimpa kopo la sabuni ya unga aina
ya omo ambalo hutoa madoa kwa uhakika

Ha ha ha ha ha ha ha ha ni janga sana.
K**a ulisoma huku ukifikiria uchawi shindwaaaaaa.........................PANSENS

news story comming soon
22/04/2017

news story comming soon

Credits:Wanaume bora na wenye hekima na busara na walio wasomi ,wanyanyekevu wenye utashi mkubwa  Wa fikra wengi wao  wa...
05/02/2017

Credits:

Wanaume bora na wenye hekima na busara na walio wasomi ,wanyanyekevu wenye utashi mkubwa Wa fikra wengi wao wamepata wanawake wasio wema na waadilifu ,tafakari kwa kina juu ya suala hili,Nelson Mandela ndoa zake zote mbili hazikudumu,Mahatma Ghandi amekufa akiwa na ndoa isiyokuwa nzuri.

Bingwa wa fasihi andishi Edwin Semzaba amekufa akiwa na ndoa isiyo na faraja wala furaha ,hakuna povu baya maishani K**a kutengeneza ndoa isiyo na furaha ,Maisha yanakuwa matamu Sana na yenye faraja K**a ukapata mke anayekupenda na wewe ukampenda kwa dhati Dunia inakuwa hazina ya furaha yenu.

Hakuna maisha mabaya K**a kuona mwanao akilelewa na Baba/Mama mwingine na wewe ukiwa bado hai sababu ya kosa uaminifu kwenye ndoa ,mtoto kukosa malezi ya mzazi mmoja anakuwa anakosa chemistry kubwa Sana ya baba na mama ,parents day huwa ni chungu sana kwa mtoto anayelelewa na mzazi mmoja pale rafiki zake wanapokuwa na baba na mama, ni wakati wa kukaa chini na kuzitawala tamaa zetu na kulea watoto wetu kwa upendo na amani.

Ukipata mpenzi sahihi daima maisha yako yatakua ya furaha, ila ukipata mpenzi bomu lazima ugeuke kuwa mwanafalsafa.

Share

Pansens..

Address

MBEYA
Tanga
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Pansens +255768 089 616 posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share