03/12/2019
MATATIZO YA JOTO KWENYE KOMPYUTA
leo ngoja tuangalie matatizo ya joto kuzidi kwenye vifaa vya kompyuta na dalili zake.
1-PSU (power supply unit)
Dalili:
A- Kompyuta inawaka taratibu mno
B-kompyuta inaganda muda ambao inaloading os baada ya kuiwasha
C-makelele kwenye feni
D-kompyuta inawaka vizuri lakini kila kitu kinakuwa ni taratibu kuliko kawaida
E-Joto kubwa mno mbele ya PC
Sababu:
A: Feni la PSU halizunguki
B:Mzunguko wa feni ni mdogo kuliko kawaida
C:Feni linazunguka k**a kawaida ila PSU yote imejaa vumbi.
2-Processor
Dalili:
A-Kompyuta kuganda
B-kompyuta inarestart bila kutoa onyo lolote
C-kompyuta haianzi
D-kompyuta inaanza taratibu mno kwenye mchakato wa kuwaka
Sababu:
Upataji joto wa Processor ambao husababishwa na yafuatayo;
(i) kupata joto Thermal compound
(ii) Ufungaji mbaya wa cooling system
(iii) matatizo ya feni
3-RAM
Dalili:
A-Hakuna picha inayoruka kwenye kioo
B-Blue screen of death(kioo kuwa cha bluu chenye maandishi )
C-OS inaganda mno.
D-program zinafanya kazi taratibu mno
E-Kioo cheusi baada ya BIOS na POST
sababu:
A-Kupatwa joto kwenye RAM module
SOMO LITAENDELEA KWENYE SEHEMU ZINGINE ZA KOMPYUTA KUSHIKA JOTO