LVRO Technology

LVRO Technology DEALERS WITH COMPUTER SERVICE, LAPTOP, PRINTER, PHOTOCOPIER REPAIR SOFTWARE AND HARDWARE INSTALLATION

I'm so grateful for having a daughter like you. Happy birthday to the world's best daughter.
02/09/2023

I'm so grateful for having a daughter like you. Happy birthday to the world's best daughter.

08/01/2015

Retweeted Clouds FM ():

Ni kweli Madalali husababisha kodi za nyumba kupanda? Na pia kwa upande wako ni muhimu kumlipa dalali hela yote... http://t.co/Hqn9vuzy70

Its new year and new appearance
01/01/2015

Its new year and new appearance

09/11/2014


Hizi habar za kuaminika, si hadithi za kakakuona,
ukifa unazikwa na kusaulika km Issa Matona, http://t.co/6FxnJKqHnE

10/09/2014

Hip Hop we ndio my Queen
my first, my last and my a very thing between

08/08/2014

Helloooooo ma man

01/08/2014

  wengi ulimwenguni wamekatishwa tamaa na watu walio karibu nao. Na mara nyingi watu hawa wanaotuzunguka siyo kwamba haw...
27/06/2014

wengi ulimwenguni wamekatishwa tamaa na watu walio karibu nao. Na mara nyingi watu hawa wanaotuzunguka siyo kwamba hawapendi maendeleo yetu bali huwa inakuwa ni katika hali ya kutulinda ili labda tusipoteze mtaji, muda au nguvu. Lakini mafanikio huja kwa sababu ya kuhatarisha (taking risk). Hivyo usiogope kuhatarisha.
Nakumbuka siku za hivi karibuni jinsi nilivyokutana na mfanyabiashara mmoja mkubwa aliyefanikiwa sana hapa jijini Dar es Salaam. Wakati milionea huyo akifanya uamuzi wa kuwekeza kwenye biashara nyingine, watu walio karibu naye walimkatisha sana tamaa na kumwambia kuwa atapoteza bure fedha zake.
Lakini kwa ujasiri akawajibu, ‘ninyi mnafikiri saaana lakini mimi ni mhatarishaji (risk taker)’. Baada ya kuyasikia hayo, nikatikisa kichwa kwa makubaliano, kisha moyoni nikajisemea, ‘ahaa, ndiyo maana mjasiriamali huyu amefanikiwa sana maishani. Ni kwa sababu, hajali watu wanasema nini. Hakubali kukatishwa tamaa kirahisi!’
Mwandishi wa vitabu vya namna ya kujitajirisha duniani k**a vile Rich Dad, Poor Dad, The Cash Flow Quadrants, Guide to Investing n.k kutoka Marekani ambaye vitabu vyake vimewatoa watu wengi gizani, aliwahi kuhojiwa katika vipindi vya televisheni na watu maarufu k**a Oprah, Larry King nk, akasema kuna watu wa aina nne katika ulimwengu wa biashara.
Aina ya kwanza ni watu ambao ni lazima wawe SAHIHI (people who must be RIGHT). Watu hawa huwa ni vigumu sana kupokea au kukubali mawazo mapya na huwa wana mrengo mmoja tu wa kufikiri. Japo watu hawa huwa hawapo tayari kuhatarisha na kufanikiwa, tunawahitaji katika nyanja nyingine maishani, mfano k**a wanasheria na wahasibu.
Aina ya pili ni watu wasiotaka USUMBUFU (people who must be COMFORTABLE). Kwa lugha nyingine ni kwamba watu hawa wako tayari kukaa sebuleni wakinywa chai, huku nyumba inaungua. Hawako tayari kuacha starehe au kutoka katika mazingira waliyonayo ili kufanya vitu tofauti au vyenye changamoto kwa kuwa hawataki usumbufu.
Aina ya tatu ni watu ambao wanataka KUPENDWA (people who must be LIKED). Kundi hili huenda na upepo. Kwa kuwa hawapendi kuchukiwa au kubishiwa, huangalia wengine wako upande gani, kisha huungana nao.
Aina ya mwisho ni watu ambao ni lazima WASHINDE (people who must WIN). Hawa huwa kinyume na hayo makundi hapo juu. Hawa ndiyo huwa miamba. Hufanya kila wanachoweza ili kufika juu maishani.
Watapambana kwa udi na uvumba mpaka wafanikiwe. Lakini jambo la muhimu sana ni kwamba wengi wa watu hawa huwa na ujasiri wa kukabiliana na aina 3 za kwanza hapo juu, kwani bila hivyo hao wa juu huhakikisha kuwa kundi hili linaungana nao na kuwa wapotezaji k**a wao katika biashara.
Je, wewe msomaji, uko kundi gani?
K**a ndiyo unaanza, fanya kila uwezalo kuwa na marafiki ambao wanapenda kushinda. Watafute popote pale, kwenye semina au makongamano, kwenye vikundi vya ujasiriamali au kusaidiana, kutoka kwa wateja au wagavi wako. Kwa namna yoyote ile, hakikisha unatafuta mabingwa, ili na wewe siku moja uje kuwa bingwa!
Kuna kitu fulani kizuri sana kuhusu kushinda maishani na katika biashara. Mabingwa hawawi mabingwa kwa sababu wameshinda. La hasha! Mabingwa wanashinda kwa sababu ni mabingwa kwanza.
Anza kujifua kadiri uwezavyo katika safari yako ya kuelekea kuwa bingwa- ili uwe unashinda maishani. Inaanza kwanza na kubadilisha mfumo mzima wa fikra, kisha inafuatiwa na kujifunza kwa bidii kila kipengele muhimu cha biashara yao. Anza leo hujachelewa!Mbinu ya pili,ni kuamua kuwa na maktaba yako mwenyewe ya mafanikio. Hii ndiyo njia nyepesi kuliko zote, kwa kuwa ni rahisi kununua vitabu kuliko kutafuta rafiki tajiri.
Anza kununua japo kitabu kimoja kwa mwezi na usome kila siku japo kwa dakika 15 k**a uko bize sana lakini k**a una muda wa kutosha, tumia nusu saa au hata saa nzima na muda mzuri ni kila asubuhi kabla hujaanza shughuli. Kufanya hivi kutakuweka mbele sana maishani kwa muda mfupi kuliko mtu asiyesoma chochote kila siku.

17/06/2014

It's all About Preventive Maintenance, Graphics Design, Web and Blogs Design

DEALERS WITH COMPUTER SERVICE, LAPTOP, PRINTER, PHOTOCOPIER REPAIR SOFTWARE AND HARDWARE INSTALLATION

14/06/2014

Address

Morogoro

Telephone

0717842190

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when LVRO Technology posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to LVRO Technology:

Share