Sharif B. Seif

Sharif B. Seif SANAA Inaishi.........KARIBU KWENYE ULIMWENGU WA FASIHI. Karibu kwenye ukurasa wangu ili tuweze kuburudika na kubadilishana mawazo kupitia fasihi.....NASEMAJE!!

Wakizipiga kwa huko wacha sie tuzicheze hapa,iwe kwa fimbo au kwa maneno na ibaki kuwa FASIHI tu.

13/02/2018

Hakuna mwanadamu aliye kamili kwa asilimia mia moja (100%) ila wapo wanadamu walio kamilika karibu ya asilimia 100 nao ni WANAO WASIKILIZA WAZAZI WAO.

Mzazi utambua kipi mwanae amepungukiwa hivyo ujitahidi kufanya vyovyote vile ili mwanae ukamilike.Mfano k**a wewe ulikamilika kwa asilimia 56 kisha yeye/wao wana asilimia 63.....watajitahidi kupunguza asilimia zao (kimawazo au kifedha) ili wewe ukamilike.

Na k**a wakikushauri usikasirike au kuwasema kwa mabaya au ata kwa kusema mapungufu yao............ndio wao ni wapungufu lakini tambua wameona mapungufu yako hivyo wanataka kuyaziba kwa zile asilimia chache za ukamilifu wao ili wewe mtoto wao uwe kamili kwa asilimia nyingi.

HESHIMU WAZAZI

👉Happy Choose Day👫👫

Nilichojifunza ni kwamba.........ukiondoa UHAI vipo vitu vingine vitatu tu ambavyo kamwe haviwezi kurudishwa (recovered)...
07/01/2018

Nilichojifunza ni kwamba.........ukiondoa UHAI vipo vitu vingine vitatu tu ambavyo kamwe haviwezi kurudishwa (recovered)

1. NENO/MANENO yanayotoka kinywani mwako wakati unaongea.

2. WAKATI kipindi ukikupita

3.MUDA pindi utakapo upoteza

Tafadhari! Jaribu sana kuwa makini na vitu hivi.


🔥

Saa 8 hii tupo uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kwaajili ya kuaga miili ya ndugu zetu,wadogo zetu,watoto zetu w...
08/05/2017

Saa 8 hii tupo uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kwaajili ya kuaga miili ya ndugu zetu,wadogo zetu,watoto zetu waliofariki kwa ajali..........maombi yataongozwa na makamu wa raisi Mh. SAMIA SULUHU HASSAN pamoja na mkuu wa mkoa wa Arusha ndugu MRISHO GAMBO

Wamdugu mliokua maeneo yako karibu tunaomba mtuwakilishe vyema,tupo pamoja katika kipindi hiki kizito....... Pumzikeni kwa Amani ndugu zetu,Amin!🙏🏼.



😪😪😪😪

JINSI YA KUKABILIANA NA MSONGO WA MAWAZO/STRESS Tafadhari soma hapa ili ulipate pumziko la akili. Watu wengi wanabeba ms...
28/04/2017

JINSI YA KUKABILIANA NA MSONGO WA MAWAZO/STRESS

Tafadhari soma hapa ili ulipate pumziko la akili.

Watu wengi wanabeba msongo wa mawazo/Stress bila kujua ni madhara gani watakayo yapata........tuchukue mfano huu kwa kuangalia hiyo picha hapo chini,tutapata kitu👇
"Ni vigumu kujua uzito wa hayo maji kwenye glasi na hata glasi yenyewe, hata kwa kushika hiyo glasi bado hautajua uzito wake (Jaribu na wewe kuishika ili hujionee)".

Umepata jibu??? HAPANA, kwanini?? Kwasababu umeshindwa kukadilia au sio?Kama umeweza kukadilia basi hauna uhakika na jibu lako si ndivyo? Sasa zingatia hiki ambacho kitakupa majibu yako;-

Uzito wa hiyo glasi na maji si kitu kwasababu hatuwezi kupata kwa urahisi isipokua hicho kitendo cha kushika glasi yenye maji ndicho majibu tosha kwetu..........ebu tujiulize vipi k**a ukishika hiyo glasi iliyokua na maji kwa dakika chache?? Jibu ni kwamba hautasikia chochote.Na vipi ukishikiria kwa lisaa au masaa??? Kipi kitatokea?? MKONO UTAUMA Ehee!,na je k**a ukishika kwa siku,wiki au Mwezi?? BILA SHAKA mkono utapooza kabisa.

Sasa nini cha kufanya?? Ni rahisi sana, cha kufanya ni kuitua hiyo glasi ya maji mkononi ili kuzuia maumivu na kupooza kwa mkono,hapo utaupa uhuru mkono wako............na hivyo ndivyo ulivyo msongo wa MAWAZO/STRESS vichwani mwetu,utakapo (u)beba kwa muda mrefu basi waweza kukuletea madhara. Nijukumu lako kuutua ili usisababishe mamumivu au madhara mengineyo kwako...........Tua huo mzigo wa mawazo/Stress,FANYA HIVYO SASA ILI KUUPA PUMZIKO UBONGO WAKO.
👍Like na Share kwa marafiki ili tupate kuondoa msongo wa mawazo/Stress.
and editting from somewhere.

18/04/2017
Like na share kwa marafiki
12/04/2017

Like na share kwa marafiki

KUHUSU SUMU YA BOTULIUM

Habari leo tujadili kidogo kuhusu sumu,najua wengi tunafahamu sumu kwa kuua viumbe hai au kuharibu viungo mbali mbali vya mwili na hata uoto wa asili hapa duniani.

Lakini je! Unafahamu sumu ilivyo kali zaidi duniani???,Sumu hatari zaidi duniani inaitwa BOTULIUM iliyoundwa kwa protein iliyotokana na bacteria aina ya CLOSTRIDIUM BOTULINUM.

Hawa nia aina ya bacteria ambao wametoka katika kundi la CLOSTRIDIUM. Wanauwezo wa kutoa sumu hii inayoitwa BOTULIUM ambayo inaathiri kwa haraka zaidi mfumo wa fahamu wa mwanadamu (Neurological).

Sumu hiyo ni kali sana kwani tone moja tu,linaweza kuua watu wazima wenye uzito wa kilogramu 50 zaidi ya milioni 26 sawa na wastani wa kuku millioni 650 kwa tone moja tu.

Like na Share kwa marafiki_Kama una swali uliza.
Kwa Elimu zaidi tukutane huku;- Knowledge-and-news.blogspot.com

Maisha yapo kasi sana...............wakati waingereza wakishangwa na BAO LA MKONO la maradona, watanzania hasa Simba fc ...
24/03/2017

Maisha yapo kasi sana...............wakati waingereza wakishangwa na BAO LA MKONO la maradona, watanzania hasa Simba fc walishangazwa na BAO LA MKONO la Tambwe.Yote yalipita ingawa yalibaki vifuani mwao (k**a dukuduku) na kichwani mwao (k**a kumbukumbu).

Ila hakuna kinachoumiza k**a "Kupata/kumpa mtu ushindi kwa BAO LA MKONO la maradona and then hao hao/yeye (w)anakupiga BAO LA MKONO la Tambwe,inaumiza sana kwakweli".................Naam!!Karibuni kwenye ulimwengu wa kabumbu Tanzania,nipo na wachambuzi wangu makini hao hapo chini. 👇👇👇





HAKI SAWASitaongelea usawa wa mwanamke kuvaa suruali k**a mwanaume,na sitaongelea usawa wa mwanaume kusuka nywele na kut...
15/03/2017

HAKI SAWA

Sitaongelea usawa wa mwanamke kuvaa suruali k**a mwanaume,na sitaongelea usawa wa mwanaume kusuka nywele na kutoboa pua k**a mwanamke.............hapa nazungumzia usawa unaofichwa chini ya kweli, ambao unaonekana kwa jicho la tatu tu.
M/mungu alimuumba Hawa'a/Eve (mwanamke) toka kwenye mbavu kuume kwa Adam (Mwanaume) kwa lengo moja tu:-
Kufanya vile vitu vyote ambavyo Adam(mwanaume) hawezi kufanya,wengi wanalazimisha ambao haupo kabisa. wa kum'bebesha gunia la misumari mwanamke, wa kumvisha viatu vya chuma mwanaume....na ndio huu wa kubadili majukumu ya k**e kwa kiume na kiume kwa k**e(wao wataona kawaida).

MUHIMU:-

Kila mtu (mwanamke/mwanaume) atambue ni yapi anaweza kufanya kwa nafasi yake na ni yapi hawezi kufanya,kwa yale asiyoweza kufanya hayaache kamwe hasifosi kuyafanya maana yupo anayeweza kubeba hayo majukumu.........ili gari hiitwe gari na iweze kutembea basi,Injini ifanye kazi yake,Mafuta yafanye kazi yake,breki zifanye kazi yake,matairi yafanye kazi yake,usukani ufanye kazi yake n.k

Hivyo ndivyo ilivyo kwenye familia,mwanamke afanye kazi yake na mwanaume afanye kazi yake...usawa huu unahitajika ili kupata kizazi bora.MUNGU BARIKI USAWA HUU.

KWA WAPENDA FASIHI TU ( kwa like,comments na share yako itampa nguvu mwanafasihi wetu,fanya hivyo sasa)SHAIRI: MVUVIFANA...
26/02/2017

KWA WAPENDA FASIHI TU ( kwa like,comments na share yako itampa nguvu mwanafasihi wetu,fanya hivyo sasa)

SHAIRI: MVUVI
FANANI: HAMZA A. MOHAMMED

Macho k**a dege bundi, Mvuvi hakuogopa
Akangiwa na tamaa, Na kutaka kulifuma
Hakutaka kufa njaa, Kalivamia kwa nyuma
Mvuvi kakak**aa, Kudunga bila huruma

Akawacha vidagaa, Kwa papa la nyamanyama
Hakuweza kulibeba, Mvuvi kaliburuza
Papa kubwa limeshiba, Kakataa kuliuza
Jitumbo k**a kiriba, Mara likamchukiza

Kalitumbua kwa miba, Uzito kulipunguza
Kufika nalo nyumbani, Chini akalitandaza
Kapasua mpaka ndani, Damu likampakaza
Wakagomba majirani, Shombo limewachukiza

Papa halina thamani, Mvuvi kalipuuza
Mvuvi kasikitika, Akaishiwa na hamu
Baada ya kulipika, Kumbe halina utamu
Kang’ang’ana kulishika, Sasa anajilaumu

Fumbo limeshasikika, Mng’amue ng’amu ng’amu
Mvuvi kala yamini, Dira hatoipoteza
Akirudi baharini, Atavua japo pweza
Nyama yake ilaini, Ukila inateleza

Fumbo nimelibaini, Fumbua k**a waweza

**Mmh!! haya kazi kwako mwanahisimu,k**a wataka kufumbua fumbo la kigogo Hamza nitanabahishe kupitia:-
(Whasapp/sms tu) +225652 688 865

WHO AM I???I am a large Animal.Change one letter and I am a dwelling.Change another letter and I am  a very small Animal...
22/02/2017

WHO AM I???

I am a large Animal.Change one letter and I am a dwelling.Change another letter and I am a very small Animal.Remove one letter and I am a River.Finally Change one letter and I am an Electrical Device. What did I finally come?

1. Bulb
2. Fuse
3. Wire

👉Like,comment ur answer and then share.

Cc:
Ni kwa watasha tu......lugha ya nyumbani ni mtihani kupata jibu,alafu kila nikitaka kutafsiri usingizi unanipiga Kofi la machoni (😂😂Shikamoo kienglish)

HIVI NDIVYO NINAVYOISHI NA WATOTO WA MJOMBA.Nilipokua kitandani niliamshwa na kelele zao,eti oooh! Bora   (J) alikua ana...
15/02/2017

HIVI NDIVYO NINAVYOISHI NA WATOTO WA MJOMBA.

Nilipokua kitandani niliamshwa na kelele zao,eti oooh! Bora (J) alikua anacheza vyema namba nne(4) licha ya kuonekana mdhaifu kwa mashabiki...........lakini si huyu (M) anayecheza kwa ubabe beki namba 5.

Unajua kwanini??? Maduhu hakuangalia rika la anaocheza nao,wala hakujua kucheza kistaharabu,ukikatisha kwake anakukanyaga tu au kukulamba mtama......wala hakujua k**a kuna faulo au hata kuiletea madhara timu yake either kwa kadi nyekundu au faini kwa fujo zake,nilimsikia akiwatisha tena akibwatuka kwa ukali "eti mpira nimefuma mimi mkiniudhi tuuuuu (......................)"

NAMJUA MIMI,ndio maana nilitabasamu kuwasikia wakimsema,haya wacha niendelee kulala maana nawajua watoto wa MJOMBA watasahau tu na kesho watampanga tena MADUHU kwenye first eleven au kumkumbuka endapo hawatampanga tena.

Source:
Mimi


Alitupa macho,wacha tukubali na miwani ya mbao.......ila kwa TANZANIA YA VIWANDA tutawapima kwa sauti za makofi yao. "Tu...
13/02/2017

Alitupa macho,wacha tukubali na miwani ya mbao.......ila kwa TANZANIA YA VIWANDA tutawapima kwa sauti za makofi yao.



"Tunalenga kutengeneza kiwanda cha simu Tanzania ambacho kitakuwa kinatengeneza simu za bei ndogo, kitasaidia wale wanaopenda simu za bei rahisi" - Waziri wa Viwanda, Charles Mwijage

Toa maoni yako

Source:
Eatv

Address

Morogoro

Opening Hours

Monday 06:30 - 00:30
Tuesday 06:30 - 00:30
Wednesday 06:30 - 00:30
Thursday 06:30 - 00:30
Friday 06:30 - 00:30
Saturday 06:30 - 00:30
Sunday 06:30 - 00:30

Telephone

0652688865

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Sharif B. Seif posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Sharif B. Seif:

Share