19/04/2026
Post yenye maana sana kutoka kwa mtu wa maana sana Mwenyezi Mungu akubariki kiongozi
USIISHIE NJIANI, WEMA MWINGI, ILA BADO MAWE MENGI!
Yesu akawaambia, “Nimewaonesheni KAZI NYINGI kutoka kwa Baba (Nimewafanyia MAMBO MENGI MEMA). NI IPI kati ya HIZO inayowafanya MNIPIGE MAWE?” (Yohana 10:32)
Mungu akupe NGUVU kuvumilia pale unapopigwa mawe bila kujali WEMA ULIOFANYA. Pamoja na yote ambayo YESU aliyafanya, ALIISHIA KUPİGWA MAWE, hadi ikabidi AWAULIZE!!!
Unaweza kujitoa sana kwa ajili ya ndugu zako, UKAJINYIMA, ukaingia kwenye MADENI. Cha Kushangaza mwishoni unaishiwa kulaumiwa na kuonekana HAUJALI ndugu. Unaweza hata kuwekewa VIKAO na kusemwa VIBAYA. MAWE!
Uliamua uache kila kitu ili umsapoti mpenzi/mwenzi wako. UKASIMAMISHA maisha yako ukiamini unachokipigania ni cha KWENU WOTE, kumbe ni cha kwake. Amekusahau, anafaidi na wengine na ANAKUTANGAZA VIBAYA.Leo wewe umegeuka si KITU kabisa. MAWE!
Wewe ni KIONGOZI pale OFISINI kwako, kwenye KIKUNDI au kwenye JAMII yako, unafanya MENGI kwa ajili ya unaowaongoza. Unajitoa, unajinyima usingizi na hata imehatarisha AFYA YAKO. Mwisho wa siku, haya yote HAYAONEKANI, unaishia KUTUKANWA na KUSINGIZIWA mabaya yanayokuchafua zaidi. MAWE!
Ndio dunia tunayoishi, sio kila anayepigwa MAWE amekosea. Sio kila unapopigwa MAWE umefanya MABAYA, hata MITUME waliotutangulia walikutana na hili.
Kikubwa, USIACHE KUFANYA MEMA kwa sababu ya wachache wanaokupiga MAWE. Nakuombea MUNGU AKUPE NGUVU na UVUMILIVU.
Nakutakia Jumapili Njema.
See You At The Top
Joel Arthur Nanauka
TIMIZA MALENGO YAKO