Digital Power

Digital Power Karibu "DIGITAL POWER" Karikoo Aggrey na Lipoma.

Ukiwa Akiba Bank unashuka kurudi kwenye mataa ya Gerezani, Jengo la kwanza Jekundu unaliacha, Jengo la pili la bluu lenye matangazo ya Tecno unaingia ndani mlango namba tano kulia kwako.

Jana December 5, 2023 ilikua ni Siku ya Kujitolea kimataifa kufanya kazi bila ya Malipo katika sekta ya kiuchumi na maen...
06/12/2023

Jana December 5, 2023 ilikua ni Siku ya Kujitolea kimataifa kufanya kazi bila ya Malipo katika sekta ya kiuchumi na maendeleo ya Kijamii “Economic Sector and Social Development “ Je umewai kujitolea au kufanya jambo lolote Lile bila ya kutegemewa kulipwa ili unachofanya kiwe ni kwa faida ya watu waliokuzunguka na Jamii yakoo kwa Ujumla?

Mimi na Marafiki zangu kwa namna moja au nyingine tumekua tukitenga mda wetu kidogo na kujitoa japo kwa uchache kwa ajili wa Wengine. matamanio yetu siku zote imekua ni kuona tunapata mabadiliko chanya kwenye changamoto mbalimbali ambazo zinaiikabili Jamii yetu. Binafsi safari yangu ya kujitoleaa ni ya takribani miaka kumi sasa kuanzia kule Muungano Secondary nikitumia sanaa ya uandishi. Baadae pale chuo kikuu cha Iringa nikiwa kwenye Asasi Mbalimbali ndani ya Chuo na Zingine nje ya Chuo

2014 tulikua kule Iramba kwa Mwigulu Nchemba tukisaidia Mradi wa Maji na Afya, nakufundisha mashuleni namna ya kutumia rasilimali zinazowazunguka kutengeneza vitu ambavyo vinaweza kurahisisha maisha yao k**a vile majiko ya kisasa, baadae tukaenda Ndala Shinyanga na Bariadi katika mradi wa Watoto chini ya Shirika la Save the Children wakishirikiana na Raleigh international

Kwa kujitolea nimehudumu kwenye Asasi mbalimbali kwa namna moja au nyingine kwa kufanya kazi bila ya malipo K**a Raleigh Tanzania wakishirikiana na Restless Development na VsO, Raleigh Tanzani Societ, Save the Children, World Merit, Tengeneza Generation Kule Gifted Heart Kaka Mkubwa Malisa GJ ametuongoza vyema sana kujitoa kwa kiasi chetu kwa watu mbalimbali na bado anafanya kazi nzuri sana kwa kugusa jamii kwenye nyanja nyingi k**a ambayo juzi imeongora hamasa ya kuchangia Damu kwa wakazi wa Dodoma

Pia Kuna hatua nyingi tumechukua na marafiki zangu na watu wanaonizunguka hapa Kariakoo k**a vile kuchangisha fedha kwa ajili ya matibabu ya watoto, Chakula cha Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu, na fedha kwa ajili ya vitabu mbalimbali amabvyo vitawasaidia kwenye masomo na harakati zao, yapo mengi japo kuyakumbuka yote kwa Pamoja inaweza kua ni ngumu

Kwenye kujitolea kuna changamoto k**a ilivyo sehemu nyingine za kazi za malipo lakin swali moja ambalo linatutatiza kila wakati baadhi ya watu wasipojitoa kwa ajili ya wengine wasio na uwezo wa kupaza sauti juu ya yale yanayowatatiza nani atafanya hivyo? Watoto na watu wengine ambao wanakua wamekata tamaa huku wanapigania afya zao kitandani nani atafanya hivyo? Kuna watoto yatima na walio kwenye mazingira magumu wakati mwingine wanakosa ada na chakula kukiwa hakuna mtu wa kuwasemea nani atafanya hivyo…

Changamoto za Kujitolea ni nyingi wakati mwingine watu wengi wanadhani ili ujitolee kusaidia kundi flan kwenye Jamii pengine unapaswa kua hauna shuhuli maalumu ya kufanya Dhana hii inapaswa kubalika haiendani kabisa na Lengo na Kujitolea kwa jamii yako kwa kua lengo la kujitolea ni kuchochea mabailiko chanya kwenye Jamii. Ukiona mema ya kujitolea na faida zake kwa wahusiika basi utapata nguvu ya kuendelea kujitolea bila kujali unapitia changamoto gani…

Kujitolea sio sehemu ya kutafuta Sifa au kujikweza ni sehemu ya Kutatua changamoto za Watu. Helen Dyer anasema Kujitolea ni Kufanyia kazi vilio vya watu kwa matendo. Matendo haya yanaweza kuharakisha matokeo chanya kwenye jamii yako. Mwaka huu December 2023 mimi pamoja na Marafiki zangu hapa Kariakoo tumejitolea kukusanya Fedha kwa Ajili ya Watoto wanaozaliwa na Mgongo wazi na Vichwa vikubwa, fedha hizi zitaelekezwa moja kwa moja kwenye matumizi ya BIMA ya Afya…

Binafsi niwapongeze watu wote ambao mmekua mstari wa mbele kusaidia wasio na sauti, wenye uhitaji, mmetenga mda wenu na kuutumia kwa ajili ha wengine Baba yenu wa mbinguni atwalipia kazi jii ambayo mnaifanya kwa mioyo yenu bila kuwaza kabisa namna mtakavyonufaika nawatakia maandilizi mema ya Xmass na Mwaka Mpaya 2024

Nawasilisha Ndahani N. Mwenda Happy Wa Joseph Christopher Cyrilo

Tembelea digitalPower ukipatie inPods yenye ubora wa Juu
04/07/2021

Tembelea digitalPower ukipatie inPods yenye ubora wa Juu

Mzigo mpya
24/05/2021

Mzigo mpya

14/04/2021

Tunawatakia waislamu wote mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

31/12/2020

inawatakia heri ya Siku kuu ya mwaka mpya 2021 ahsanteni kwa kutuunga mkono kwa kipindi chote

Mdundo kabambe   tupigie +255758154243‬ au tutembeee agrey na likoma kariakoo
23/11/2020

Mdundo kabambe tupigie +255758154243‬ au tutembeee agrey na likoma kariakoo

20/10/2020
14/10/2020

Leo 14 October, 2020 inaungana na watanzania wote katika kumbukizi ya miaka 21 ya kifo cha mwanzilishi na Mpigania uhuru wa Tanganyika (Sasa Tanzania) Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julias Kambarage Nyerere. Tudumishe amani na mshikamo

  ni suluhisho la vifaa kwa ajili ya simu yako tutembelee Kariakoo Aggrey na Likoma au tupigie/WhatsApp 0758154243      ...
11/10/2020

ni suluhisho la vifaa kwa ajili ya simu yako tutembelee Kariakoo Aggrey na Likoma au tupigie/WhatsApp 0758154243 na Pembe yote ya kokote tunakufikia

05/10/2020

Katika wiki hii ya huduma kwa wateja tunasema ahsante kwa kua sehemu ya wateja wetu, tunakuahidi ushirikiano na huduma nzuri kutoka kwetu. Tunakutakia wiki njema ya Huduma kwa Wateja. tupigie/WhatsApp 0758154243

Jipatie chaja kwa ajili ya simu yako fika aggrey na likoma au tupigie/whatsApp 0758154243 popote Tanzania tunakufikia   ...
30/09/2020

Jipatie chaja kwa ajili ya simu yako fika aggrey na likoma au tupigie/whatsApp 0758154243 popote Tanzania tunakufikia na pembe yote ya

Karibu   ujipate vifaa kwa ajili ya simu yako tupigie/whatsApp 0758154243
19/09/2020

Karibu ujipate vifaa kwa ajili ya simu yako tupigie/whatsApp 0758154243

Address

Lipoma Street
Dar Es Salaam

Telephone

+255758154243

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Digital Power posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share