20/03/2026
Ilikuwa alasiri ya Jumamosi, katikati ya Dar es Salaam.
Wafanyabiashara wawili — Penzila na Japhet — walikuwa wanauza mpango wa kupunguza uzito. Waliuza bidhaa inayofanana, Na Walilenga wanawake wanaotaka kupunguza uzito.
Wote waliweka tangazo la kulipia Facebook.
Lakini kilichotokea… kilishangaza.
Penzila alikuwa bize sana:
📲 Kujibu DMs muda wote
📲 Kujielezea kwa maneno marefu mteja akija WhatsApp
Alipost: “Mpango wa kupunguza kilo 5 ndani ya siku 30, bila Gym — Tsh 50,000 tu.”
Aliwapeleka watu moja kwa moja WhatsApp. Ambapo Walianza kuuliza…
👉 “Imetengenezwa na nini?”
👉 “Ninaweza kuacha vyakula gani?”
👉 “Inafanya kazi kweli?”
Halafu… wanapotea. Hawakununua.
Japhet yeye alikuwa kimya. Amekaa pembeni, akitazama PC yake kwa utulivu huku akinywa kahawa.
Kila baada ya dakika kumi…
📩 “New lead captured.”
📩 “New lead joined WhatsApp Group.”
Tofauti ?
Japhet hakuanza kuuza. Alianza na kuwasaidia wateja wake kwanza.
Alitengeneza chambo moja tu:
“Pakua ebook ya bure: Vyakula 10 vya Kuacha Mara Moja K**a Unataka Kupunguza Uzito.”
Hakuweka maneno mengi, wala kushawishi.
Ilikuwa k**a first aid kwa mtu mwenye tatizo. Tangazo lake lilienda kwenye Landing Page, si WhatsApp moja kwa moja.
Landing page:
• Haikuwa ikiuza mpango wowote
• Haikuwa na story ndefu
Kazi yake: Kukusanya jina na namba ya mteja.
Mteja anajaza fomu, anapakua ebook, na kujiunga kwenye WhatsApp Group ya Bure. Simple.
Ndani ya WhatsApp Group: Japhet alifundisha
1. Elimu rahisi kuhusu uzito
2. Makosa yanayofanya watu washindwe kupunguza kilo
3. Majibu ya maswali
4. Ushuhuda mdogo
5. Follow-up za kimfumo
Watu walijifunza, wakamwamini. Walipoanza kupata matumaini, Japhet akaanza kuwauzia bila kuwasukuma:
“K**a ungependa mpango kamili wa kupunguza uzito, huu ndio mpango wangu.”
WALINUNUA.
Kwa nini?
• Walikuwa tayari wanamwamini
• Wameshaona matokeo madogo
• Tayari kisaikolojia
Penzila alikosea hapa:
1. Alitaka kuuza kwanza,
Kwenye biashara mtandaoni, watu hawanunui siku ya kwanza.
Wananunua baada ya:
• Kuamini
• Kuelewa
• Kujiona wako salama
Kwa hiyo, k**a unauza mpango, huduma, training, au program yoyote: Usianze kuuza, toa kitu cha BURE KWANZA.
Wape imani,alafu wauzie.