WashaData Ujifunze

WashaData Ujifunze Ili Ufanikiwe kimaisha ni lazima ufanye kwanza uwekezaji ndani ya Ubongo wako ndipo uanze kuchukua hatua za kusonga mbele. Je ubongo wako umeulisha nini?

utajifunza Biashara,Teknolojia, Online deals.

Unaweza kununua Mkoba huu Kwa Laki 6 Tu 😂😂.Ni vigumu kuona kwa macho ya binadamu. Mkoba huu una rangi ya manjano-kijani ...
30/06/2023

Unaweza kununua Mkoba huu Kwa Laki 6 Tu 😂😂.

Ni vigumu kuona kwa macho ya binadamu. Mkoba huu una rangi ya manjano-kijani yenye kung'aa na umetokana na muundo maarufu wa mbunifu wa mavazi, Louis Vuitton - ingawa ni kazi ya kikundi cha sanaa huko New York, Marekani.

Mkoba mdogo sana ambao una kipimo cha takriban milimita 657 kwa 222 kwa 700 (au chini ya inchi 0.03 kwa upana) uliuzwa katika mnada mtandaoni siku ya Jumatano.

ChukuaHiiPovu la chura linaweza likatibu majeraha ya wagonjwa walioungua moto. Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa n...
29/10/2022

ChukuaHii

Povu la chura linaweza likatibu majeraha ya wagonjwa walioungua moto. Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Strathclyde cha Scotland.

Povu hilo gumu lenye urefu wa sentimeta tano ambalo hutolewa na vyura wanaopatikana katika kisiwa cha Tungara huko Trinidad kwa ajili ya kulinda mayai yao dhidi ya magonjwa na hali ya hewa kwa wastani wa siku tano, linaweza kukusanywa na kutumiwa katika mchakato wa matibabu kwa binadamu k**a kizuizi baina ya bandeji na ngozi iliyoungua.

Dkt. Paul Hoskisson na wenzake wanasema wameweza kuzichunguza aina nne za protini zinazopatikana katika povu hilo na tayari wameanza kuzichanganya na dawa zao.

Darby Ambayo Haiti Sahaulika. 😳😳😳Derby ambayo imepelekea watu 127 kupoteza maisha... Tukio la kusikitisha katika histori...
02/10/2022

Darby Ambayo Haiti Sahaulika. 😳😳😳

Derby ambayo imepelekea watu 127 kupoteza maisha...
Tukio la kusikitisha katika historia ya soka, mapigano yalizuka kati ya mashabiki wa soka nchini Indonesia, kati ya mashabiki wa Arema na Persebaya Surabaya, na hiyo ilikuwa Derby ambayo ilimalizika kwa Persebaya Surabaya walikuwa ugenini kuibuka na ushindi wa 3-2.

Kwa mujibu wa "GOAL" ni kuwa tukio hilo lilianza kwa mashabiki wawili kuingia uwanjani, na kisha maelfu ya mashabiki kujumuika nao mpaka kupelekea hali kuwa mbaya zaidi uwanjani licha ya kwamba mechi ilikuwa imemalizika tayari.

Baada ya mashabiki wengi kuingia uwanjani polisi wa kaanza kufyatua mabomu ya machozi kuwatawanya maelfu ya mashabiki waliokuwa uwanjani hapo, pamoja na kurusha mabomu ya machozi katika majukwaa.

Jambo ambalo lilifanya hali kuwa mbaya zaidi, kwani mashabiki waliingiwa na hofu, na kuanza kutafuta sehemu ili kujiokoa

Kulingana na ripoti kadhaa za vyombo vya habari vya Indonesia, idadi ya waliofariki imefikia 127 kutokana na ajali hiyo ingawa huenda idadi ya waliofariki ni kubwa zaidi.

📸 : TW / TRTWorldNow

28/09/2022
Faiza Ally; ni staa wa Bongo Movies na mjasiriamali wa Bongo ambaye ametoa mazito akisema kuwa, pamoja na kwamba hajasom...
09/09/2022

Faiza Ally; ni staa wa Bongo Movies na mjasiriamali wa Bongo ambaye ametoa mazito akisema kuwa, pamoja na kwamba hajasoma, lakini amewapita wasomi wengi.

Faiza anasema; “Nimezaliwa miaka 38 nyuma kutoka mtaani mpaka nilipo leo, sina jina la baba, mama wala elimu yoyote, sina urithi wa wazazi wala sitegemei wa mume…kwa hiyo maisha yangu hayakuwa rahisi, sura yangu isikudanganye.

“Halafu nimewapita wasomi wengi tu na baba zao na mama zao na waume zao na wake zao kuanzia sura zao mpaka maisha yao, wenye hela na majina...sura yangu au maisha yangu usichukulie poa…nyuma yake kuna mishale mingi sana naendelea kukwepa.
“Machungu mengi na furaha na mfanikio pia … K**a unavyojua maisha yalivyo magumu na bado mbishi, kwa hiyo vitu vya hovyohovyo havinishtuagi….”

Chukua hii✍️Kitendo cha nyoka  Kujivua Magamba kitaalam kinaitwa Sloughing. Zipo sababu kuu mbili ambazo zinapelekea Kuf...
19/08/2022

Chukua hii✍️

Kitendo cha nyoka Kujivua Magamba kitaalam kinaitwa Sloughing.

Zipo sababu kuu mbili ambazo zinapelekea Kufanya hivyo.

Sababu ya kwanza ni kuruhusu Ukuaji wa mwili wake lazma atoe ngozi yake ya zamani ili kuruhusu ukuaji Wake.

Sababu ya pili, hii hufanywa na nyoka majike tu wanapokua kwenye estrus yaani Wanapokua tayari kuzaliana ili jike ampe taarifa dume kuwa yupo tayari kwa kukutana basi hujivua magamba ili kuruhusu kuachiwa kwa harufu fulani ya wali.

Ndiyo maana kuna sehem ukipita hasa maeneo yenye vichaka unaweza Kuipata hii harufu ya wali, hapo utamsikia mbongo akisema "majini Wanapika Wali sehemu hii tuondoke haraka sana 😄😄" kumbe nyoka nyupo kwenye harakati za kumvuitia baby wake 🥰

Basi tambua kuwa hiyo harufu hutolewa na Jike la nyoka kuashiria yupo tayari kukutana na nyoka dume.✍️

  kwa awamu ya pili imeachisha kazi takriban Wafanyakazi 300 k**a namna ya kudhibiti gharama za uendeshaji. Mnamo mwezi ...
24/06/2022

kwa awamu ya pili imeachisha kazi takriban Wafanyakazi 300 k**a namna ya kudhibiti gharama za uendeshaji. Mnamo mwezi Mei ilipunguza Wafanyakazi takriban 150

> Kampuni hiyo imedaiwa kupoteza Watazamaji 200,000 mwaka huu


Hii ni Sanamu ya Bastola Iliyokunjwa. Sanamu hii inpatikana katika ofisi ya Makao Makuu Ya Umoja Wa Mataifa huko New Yor...
24/06/2022

Hii ni Sanamu ya Bastola Iliyokunjwa. Sanamu hii inpatikana katika ofisi ya Makao Makuu Ya Umoja Wa Mataifa huko New York City.

Alama hii ni Ya kuwakilisha Amani Ulimwenguni.

 : Tumia USB zisizoruhusu taarifa kuhama kutoka kwenye simu yako kwenda kwenye chombo kingine > Ukitumia USB inayoweza k...
21/06/2022

: Tumia USB zisizoruhusu taarifa kuhama kutoka kwenye simu yako kwenda kwenye chombo kingine

> Ukitumia USB inayoweza kuhamisha mafaili chagua "Option" ya "Charge Only" na uifunge simu yako ili kuzuia uhamishaji wa data zako

Mara nyingi watu wenye akili hutambulika kwa mambo mengi, ikiwemo namna anavyofikiria na kufanya maamuzi, maendeleo yake...
20/06/2022

Mara nyingi watu wenye akili hutambulika kwa mambo mengi, ikiwemo namna anavyofikiria na kufanya maamuzi, maendeleo yake, namna ambavyo anaweza kutatua changamoto kwa uharaka na usahihi, lakini pia namna ambavyo anaweza kuwa msaada kwa wengine.
Binadamu huzaliwa na akili lakini kiwango cha akili kwa mtu mmoja na mwingine hutofautiana kutokana na sababu nyingi, japokuwa kisayansi sababu huanzia huanzia tangu pale mimba inapotungwa hadi mtoto anapozaliwa.
Akili zinaweza kurithiwa au kupatikana kutokana na mazingira pamoja na maishi unayoishi, kwa mujibu wa wataalamu, mazingira yanayokuzunguka yanaweza kuathiri uwezo wa ubongo wako na namna ambayo unafikiria, na kuchukua maamuzi katika maisha unayoishi.

mujibu wa wataalamu wamebaini kuwa watu wote wenye akili huwa na tabia zinazofanana na pia huwa na vitu vingi vinavyoendana.
Taarifa zilizokusanywa na watafiti, Bright Side wamechambua mambo 9 ambayo watu wenye akili huyafanya k**a ifuatavyo
1. Hawapendi kufanya umbea, tafiti zinaonesha wanapenda kuwa wapweke japokuwa haimaanishi kuwa ni wapweke (loners) bali wanapenda kupata nafasi ya kufikiria zaidi.
2. Wanapenda kuchekesha/kufurahisha watu wengine, wana uwezo mkubwa wa kugeuza jambo lolote na kuwa la kufurahisha.
3. Wanapenda kuongea wenyewe, mwanasayansi Albert Einstein alikuwa na tabia ya kuongea mwenyewe.
4. Wanapenda kusikiliza muziki mara nyingi, wanapenda kuwa na spika za masikioni (Earphones) muda wote, inaelezwa pia wanapenda kusikiliza nyimbo zisizo eleweka wanapendelea kusikiliza biti kuliko mashairi.
5. Hufanya kazi kwa umakini na sio kutumia nguvu kubwa, wana tabia za uvivu na hiyo ndio huwafanya kupenda kutaka kurahisisha vitu mbalimbali.
6. Wanapenda kujifunza na kutafuta majibu ya kila changamoto wanayokumbana nayo, hupenda kusoma sana vitabu na kuwela kumbukumbu ya mambo yao katika diary.
7. Wanakubali kirahis pale wanapoona wamekosa
8. Wanapenda kula sana chokoleti
9. Hawapendi kuongea sana, wanapenda kuongea pale wanapoona inafaa kwa muda huo, endapo kutatokea majibizano hawapendi kujihusisha nayo.

Share na wengine

Je wajua chimbuko la siku ya baba (father's day)?Siku ya baba ilianzia huko Marekani ambapo inasadikiwa mwanamke Sonora ...
19/06/2022

Je wajua chimbuko la siku ya baba (father's day)?

Siku ya baba ilianzia huko Marekani ambapo inasadikiwa mwanamke Sonora Dodd kutoka Washington alijiuliza kwanini kusiwe na siku ya baba k**a kuna siku ya mama. Sonora na wadogo zake walilelewa na baba baada ya mama yao kufariki wakati wa kujifungua.

Grace Clayton kutoka West Virginia naye anasadikika kuchangia wazo la siku ya baba. Baada ya mgodi kulipuka na kuua wanaume 350 huku zaidi ya 200 wakiwa ni baba. Hivyo akaona ni vyema kuwe na siku ya baba ambapo watoto wangepata fursa ya kuwaenzi baba zao waliofariki.

Hizo ndiyo nadharia za kuanzishwa kwa siku ya baba ambapo inasemekana imekuwa ikisherehekewa katika nchi mbalimbali kwa zaidi ya miaka 100 ama zaidi iliyopita.

K**a ulikuwa hujui YOU’RE WELCOME!!

Happy Father's Day to all great fathers out there...😘😘😘

Follow 👉👉 Nitamlea

Address

Dar-es-salaam Institute Of Technology
Dar Es Salaam
T.ENGINEERING

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when WashaData Ujifunze posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share