Mohamed Hafidh Tz

Mohamed Hafidh Tz Tech Wiz πŸ‘¨β€πŸ’» | Designer 🎨 | Coder ⌨️
Fueling minds with:
πŸ₯‡Education
πŸ₯ˆEngagement
πŸ₯‰Entertainment
Sharing my passion for creativity & innovation.

Wiki iliyopita ilikuwa wiki nzuri sana. πŸš€Videos 5, posts 2… na zaidi ya hapo, watu waliosimama kusupport, ku-comment, ku...
04/09/2026

Wiki iliyopita ilikuwa wiki nzuri sana. πŸš€

Videos 5, posts 2… na zaidi ya hapo, watu waliosimama kusupport, ku-comment, kushare na hata kunitumia ujumbe. ❀️

Likes 183
Shares 276
Comments 23
Na zaidi ya 5.7K people walifika kwenye content yangu.

Kitu ninachokipenda zaidi sio hizi numbers pekee, bali kuona kwamba kile ninachoshare kinafika kwa watu na kuwafanya washiriki.

Kila video ninayoweka, kila post ninayotengeneza na kila idea ninayoshare ni sehemu ya safari yangu ya kujifunza na kukua pamoja na ninyi.

Na honestly, 276 shares imenifurahisha sana. πŸ₯ΉπŸ”₯
Kwa sababu mtu akishare content yako, maana yake ameona kuna kitu ndani yake ambacho kinaweza kumsaidia au kumvutia mtu mwingine.

Hii ni wiki moja tu.
Tunaendelea. πŸ’ͺ🏽

Asante kwa kila mmoja anayekuwa sehemu ya safari hii. ❀️

Na wewe, wiki yako ilikuwaje?
Umefanikisha kitu gani ambacho unajivunia wiki iliyopita? πŸ‘‡πŸ½

Thumbnail yako inaweza kuwa sababu mtu akaamua kubonyeza video yako… au akaipita kabisa. πŸ‘€Watu wengi wanaweka muda mwing...
04/09/2026

Thumbnail yako inaweza kuwa sababu mtu akaamua kubonyeza video yako… au akaipita kabisa. πŸ‘€

Watu wengi wanaweka muda mwingi kwenye video yenyewe, lakini wanasahau kitu kimoja muhimu: thumbnail ndiyo first impression ya video yako.

Thumbnail nzuri si lazima iwe na vitu vingi. Inatakiwa iwe clear, readable na imwambie mtazamaji kwa haraka video inahusu nini.

Kitu kingine nilichojifunza ni kwamba usiangalie thumbnail yako peke yake. Iangalie ikiwa imekaa pamoja na thumbnails za video nyingine zinazoshindana nayo. Je, yako inaonekana? Je, inavutia macho? Je, inamfanya mtu awe curious kujua zaidi?

Na zaidi ya yote, tafuta style yako.
Rangi, fonts, faces na aina ya design unayotumia mara kwa mara vinaweza kuwafanya watu wakuitambue hata kabla hawajasoma jina la channel.

Kwa kifupi:
πŸ‘‰ Keep it simple
πŸ‘‰ Tumia text inayosomeka hata kwenye screen ndogo
πŸ‘‰ Tumia picha zenye quality
πŸ‘‰ Tengeneza curiosity
πŸ‘‰ Jenga style ambayo watu wataitambua

Thumbnail si mapambo ya video. Ni sehemu ya video inayouza click. 🎯

Swipe kwenye carousel uone baadhi ya tips na mifano niliyoweka. πŸ‘‰

Wewe huwa unatengeneza thumbnail zako mwenyewe au unatumia designer? πŸ‘‡

27/08/2026

Cybersecurity ni nini hasa? Na k**a unataka kuanza kujifunza Cybersecurity, unatakiwa kuanzia wapi?

Watu wengi wakisikia Cybersecurity wanafikiria hacking, Kali Linux, Nmap na commands nyingi. Lakini Cybersecurity ni kubwa zaidi ya hapo.

Katika video hii utaelewa kwa lugha rahisi:
πŸ” Cybersecurity ni nini?
πŸ›‘οΈ Cybersecurity inalinda vitu gani?
πŸ”Ί CIA Triad ni nini?
🌐 Cybersecurity ina tofauti gani na Network Security?
πŸ‘¨β€πŸ’» Hacker na Cybersecurity vina uhusiano gani?
πŸ›‘οΈ Defensive Security na Offensive Security ni nini?
πŸ’Ό Kuna career paths gani ndani ya Cybersecurity?
πŸš€ Na k**a wewe ni beginner, unapaswa kuanzia wapi?

Jambo muhimu zaidi ni kwamba usiwe na haraka ya kukimbilia tools kabla hujajenga msingi. Kwanza elewa fundamentals, kisha jenga skills hatua kwa hatua.

πŸ“˜ Unataka kufuata Cybersecurity Roadmap hatua kwa hatua?πŸ‘‡

https://snippe.me/pay/mohamedhafidhtz

Nimeandaa Cybersecurity Roadmap kwa Kiswahili kwa mtu anayeanza safari hii na anataka kujua:
βœ… Aanze na nini
βœ… Ajifunze Networking kiasi gani
βœ… Linux aanzie wapi
βœ… Programming inahitajika kiasi gani
βœ… Security fundamentals
βœ… Web Security
βœ… Nmap, Wireshark, Burp Suite na tools nyingine
βœ… Jinsi ya kujenga Home Lab
βœ… Practical Labs & CTFs
βœ… Projects za kujenga Portfolio
βœ… Jinsi ya kuchagua Cybersecurity specialization
βœ… Portfolio na GitHub
βœ… Certifications
βœ… Career paths
βœ… Challenge ya siku 30
βœ… Roadmap ya siku 90 na zaidi

πŸ“– Pata Cybersecurity Roadmap hapa:
πŸ‘‰ https://snippe.me/pay/mohamedhafidhtz

Kitabu hiki hakilengi kukufanya ukariri commands. Lengo ni kukusaidia kujenga msingi na kufuata safari yenye mpangilio.

🎯 K**a wewe ni beginner:

Usijaribu kujifunza kila kitu kwa wakati mmoja.

Jenga msingi β†’ Fanya mazoezi β†’ Jenga projects β†’ Chagua direction β†’ Jenga portfolio.

Cybersecurity si safari ya kujua commands nyingi.

Ni safari ya kujenga uwezo unaoweza kuonyesha.

⚠️ Muhimu
Usifanye security testing kwenye systems, websites au networks ambazo huna ruhusa ya kuzitest. Tumia labs zako mwenyewe au mazingira yaliyotengenezwa kwa ajili ya mazoezi.

πŸ“Œ Video hii ni sehemu ya Cybersecurity Beginner Series

Katika videos zinazofuata tutaendelea hatua kwa hatua kujenga uelewa wa Cybersecurity kutoka msingi mpaka practical concepts.

Subscribe ili usikose video inayofuata. πŸ”

https://www.youtube.com/watch?v=ekDwHc-x6-4&t=36s

26/08/2026

Ukiwa nyumbani, simu, laptop, Smart TV na vifaa vingine vinaweza kutumia Internet kupitia Router moja. 🌐

Lakini… Router ni nini hasa?

Je, Router ndiyo Wi-Fi?
Je, Router ndiyo Internet?
Na kwa nini ukizima Router, Internet ya nyumbani inakatika? πŸ€”

Kwenye video hii tunaelezea kwa lugha rahisi:
πŸ”Ή Router ni nini na inafanya kazi gani
πŸ”Ή Jinsi Router anavyoelekeza data
πŸ”Ή Routing Table ni nini
πŸ”Ή Tofauti kati ya Router, Wi-Fi na Internet
πŸ”Ή Router anavyounganisha vifaa vyako na ISP
πŸ”Ή Private IP Address na MAC Address zinavyohusiana na Router
πŸ”Ή Router inaweza kufanya kazi bila Internet?
πŸ”Ή LAN Ports na Ethernet Cable zinafanya kazi gani
πŸ”Ή Kwa nini Router ikizimwa connection ya Internet inakatika
πŸ”Ή Safari ya data kutoka kwenye simu yako hadi kwenye server

Mwisho wa video utaweza kuelewa kwa urahisi kinachotokea nyuma ya pazia unapofungua YouTube, kutumia WhatsApp au kufanya chochote kinachohitaji Internet. πŸš€

πŸ“Œ Video inayofuata:
Tutaangalia Wi-Fi ni nini, inafanyaje kazi, na kwa nini signal yake huwa dhaifu ukiwa mbali na Router.

K**a video imekusaidia, Like πŸ‘, Subscribe πŸ”” na mshirikishe mtu mwingine anayechanganya Router, Wi-Fi na Internet.

26/08/2026

Inawezekanaje Public IP Address moja kutumiwa na watumiaji wengi kwa wakati mmoja? πŸ€”

K**a nyumbani kuna simu 5, laptop 2, Smart TV na vifaa vingine vingi, kwa nini vyote vinaweza kutumia Internet kupitia Public IP Address moja?

Hilo ndilo swali tunalolijibu kwenye video hii.

Katika video hii utaelewa kwa mfano rahisi jinsi Public IP, Private IP, Router na NAT (Network Address Translation) zinavyofanya kazi pamoja ili vifaa vingi viweze kuwasiliana na Internet kupitia Public IP moja.

🎯 Kwenye video hii utajifunza:

βœ… Tofauti kati ya Public IP na Private IP
βœ… Kwa nini vifaa vingi vinaweza kutumia Public IP moja
βœ… Router anafanya kazi gani kwenye mawasiliano
βœ… NAT ni nini na kwa nini ni muhimu
βœ… Jinsi NAT inavyotofautisha connections za vifaa mbalimbali
βœ… Mfano wa simu, laptop na Smart TV kutumia Public IP moja
βœ… Jinsi data inayorudi kutoka Internet inavyofikishwa kwenye kifaa sahihi
βœ… CGNAT ni nini
βœ… Jinsi Internet Service Providers wanavyoweza kuwashirikisha wateja wengi Public IP chache

Mfano rahisi

Simu inaweza kuwa na Private IP:

`192.168.1.10`

Laptop:

`192.168.1.11`

Smart TV:

`192.168.1.12`

Lakini vifaa vyote vinaweza kwenda Internet kupitia Public IP moja, kwa mfano:

`41.59.100.25`

Hapa ndipo NAT inapoingia na kusaidia router kufuatilia connections za vifaa mbalimbali.

Jibu kwa kifupi

Vifaa vingi vinaweza kutumia Public IP moja kwa sababu router hutumia NAT kubadilisha na kufuatilia mawasiliano ya vifaa vya ndani, huku kila kifaa kikiwa na Private IP yake.

Na katika baadhi ya mazingira, ISP anaweza kutumia CGNAT (Carrier-Grade NAT) kufanya wateja wengi washirikishe Public IPv4 address chache.

---

πŸŽ₯ K**a hujaona video yangu ya β€œIP Address ni nini?”, anza nayo kwanza ili upate msingi mzuri wa kuelewa mada hii.

πŸ‘ K**a video imekusaidia, Like, Subscribe, na usisahau ku-share na mtu mwingine anayejifunza Networking.

πŸ’¬ K**a una swali kuhusu IP Address, NAT, Router, Wi-Fi au Networking, liache kwenye comments. Huenda likawa mada ya video inayofuata.

26/08/2026

MAC Address ni nini? Na k**a kila simu au kompyuta ina IP Address, kwa nini bado tunahitaji MAC Address? πŸ€”

Hili ni swali ambalo huwachanganya watu wengi wanapoanza kujifunza Networking.

Katika video hii, nitakueleza MAC Address ni nini, kwa nini ipo, inafanya kazi vipi, na tofauti yake na IP Address kwa kutumia mifano rahisi ya maisha ya kawaida.

Katika video utajifunza:
βœ… MAC Address ni nini?
βœ… MAC Address huonekanaje?
βœ… Kwa nini kifaa kina MAC Address na IP Address kwa wakati mmoja?
βœ… MAC Address inasaidiaje router kutambua vifaa?
βœ… Tofauti kati ya MAC Address na IP Address
βœ… Je, MAC Address inaweza kubadilika?
βœ… MAC Address Spoofing ni nini?
βœ… Random MAC Address ni nini?
βœ… Je, MAC Address inaweza kutumika kumfuatilia mtumiaji?
βœ… Jinsi IP Address na MAC Address zinavyofanya kazi pamoja

Kwa kifupi:

IP Address = kifaa kinapatikana wapi kwenye mtandao
MAC Address = kifaa gani hasa

Video hii ni sehemu ya mfululizo wa kujifunza Computer Networking na jinsi Internet inavyofanya kazi, kwa lugha rahisi ya Kiswahili.

πŸ“Œ Video iliyopita: IP Address ni Nini?
πŸ“Œ Video inayofuata: Router ni Nini na Inafanyaje Kazi?

K**a umeelewa kitu kipya kupitia video hii, bonyeza Like πŸ‘, Subscribe na ushiriki video hii ili kuwasaidia wengine kujifunza Networking kwa Kiswahili.

Youtube:
https://www.youtube.com/watch?v=0xZdJCWdEeU

πŸ”Unataka kuanza kujifunza Cybersecurity lakini hujui uanzie wapi?Watu wengi wakisikia Cybersecurity wanafikiria Hacking,...
25/08/2026

πŸ”Unataka kuanza kujifunza Cybersecurity lakini hujui uanzie wapi?

Watu wengi wakisikia Cybersecurity wanafikiria Hacking, Kali Linux na Nmap… lakini ukweli ni mkubwa zaidi ya hapo. πŸ‘€

Kwenye video hii nimeeleza Cybersecurity ni nini hasa, inahusika na nini, ina career paths gani na beginner anapaswa kuanzia wapi.

πŸŽ₯ Itazame hapa:

https://youtu.be/fLwwFMHzIe8?si=0-SED-K0aigEeXqw

Usianze Cybersecurity kabla hujaelewa msingi huu.πŸ”₯πŸ”

🚨 UNAPOST YOUTUBE LAKINI VIEWS HAZIJI?Unaweza kutumia muda mwingi kurecord na ku-edit video yako, ukaipost ukiwa na matu...
16/08/2026

🚨 UNAPOST YOUTUBE LAKINI VIEWS HAZIJI?

Unaweza kutumia muda mwingi kurecord na ku-edit video yako, ukaipost ukiwa na matumaini makubwa… halafu ukiangalia YouTube Studio unaona 7 views, 12 views, au hata 5 views.πŸ˜”

Lakini swali ni hili: Tatizo ni YouTube, au kuna kitu tunakifanya vibaya? πŸ€”

Kwenye Video #01 ya series hii, nimekuonyesha sababu 7 muhimu ambazo zinaweza kuwa zinazuia videos zako kupata views β€” kuanzia topic, title & thumbnail, intro, retention, audience mpaka YouTube Analytics.

πŸ”₯ K**a unataka kuacha kubahatisha na kuanza kuelewa kwa nini videos zako hazipati views, hii video ni kwa ajili yako.

▢️ Tazama FULL VIDEO YouTube hapa:
πŸ‘‡
https://youtu.be/RZg6jCC-9x8?si=l60Xu7WD7gV1XJJ0

Na hii ni mwanzo tu. πŸš€
Video inayofuata: Jinsi ya Kuchagua Mada za YouTube Zinazoweza Kupata Views.

πŸ’¬ Ni kitu gani kinakusumbua zaidi kwenye YouTube yako β€” Views, Subscribers au Watch Time? Niacheni comment hapa chini. πŸ‘‡

K**a kweli unataka kujifunza kitu kwa undani, usiishie kukisoma tu.Jaribu kukifundisha.Unapomfundisha mtu mwingine, unal...
16/08/2026

K**a kweli unataka kujifunza kitu kwa undani, usiishie kukisoma tu.

Jaribu kukifundisha.

Unapomfundisha mtu mwingine, unalazimika kuelewa kile unachokijua kwa kiwango cha juu zaidi. Unagundua mapungufu yako, unatafuta majibu, na unajenga uelewa wa kweli.

Ndiyo maana kujifunza + kufanya + kufundisha ni combination yenye nguvu sana. 🧠πŸ”₯

Usisubiri uwe expert ndipo uanze kufundisha.
Jifunze. Elewa. Fundisha. Kua.

16/08/2026

02. Jinsi ya Kuandaa Mazingira ya jQuery (VS Code + HTML + Browser) | Beginner Course

Kabla hujaanza kuandika jQuery, ni muhimu kwanza kuandaa mazingira sahihi ya kazi.

Kwenye video hii ya jQuery Course for Beginners, tutajenga project yetu hatua kwa hatua kwa kutumia VS Code, HTML, CSS, JavaScript na Browser.

Utajifunza jinsi ya:
βœ… Kutengeneza folder la jQuery project
βœ… Kufungua project kwenye VS Code
βœ… Kuunda `index.html`, `style.css` na `script.js`
βœ… Kuunganisha CSS na JavaScript kwenye HTML
βœ… Kufungua project kwenye browser
βœ… Kutumia Live Server
βœ… Kuhakikisha CSS na JavaScript vinafanya kazi vizuri
βœ… Kutambua na kurekebisha makosa ya kawaida ya beginners

Mwisho wa video hii utakuwa na mazingira kamili ya kuanzia kujifunza na kuandika jQuery code kwenye video zinazofuata.

πŸ’‘ Kumbuka: Kwenye video hii hatujaanza kuandika jQuery bado. Tunajiandaa kwanza ili tutorial zinazofuata ziwe rahisi kufuata bila usumbufu wa setup.

πŸ“š VIDEO INAYOFUATA

Kwenye video inayofuata tutajifunza jinsi ya kuongeza jQuery kwenye project yetu kwa kutumia CDN na Offline File, na hapo ndipo tutaanza rasmi kutumia jQuery.

FANYA MAZOEZI

Baada ya video hii, jaribu mwenyewe:
Kubadilisha heading
Kubadilisha rangi
Kubadilisha background
Kubadilisha title ya browser

Ukipata kila kitu kinafanya kazi, andika "Nimefanikiwa" kwenye comments. πŸ™Œ

πŸ‘ K**a video imekusaidia, usisahau Like, Subscribe, na kuwasha πŸ”” notification ili usikose video zinazofuata.

Address

Zanzibar

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mohamed Hafidh Tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share