16/01/2024
Mashabiki sometimes watapiga kelele kwanini timu zinachukua Wachezaji walioachwa? Wachezaji waliomaliza mikataba ama wachezaji ambao wametemwa sehemu na wengine wataenda mbali kuwa labda wanatoka Ligi dhaifu ama hazina ushindani mkubwa, lakini Shabiki huyo anasahau nae ana jukumu lake la msingi.
Mashabiki wa Kariakoo hizi timu zenu haziwezi kufanya mambo k**a Mamelodi Sundowns wala Al Ahly kwakuwa ninyi hamna sifa hizo, Mamelodi anamtaka Kiungo mwingine mwenye thamani ya Billion 6.2 ukijumlisha na Marco Allende aliyepo pale ni sawa na Billion 12 ambazo ni bajeti za Simba na Yanga kwa msimu, mwenzako kalipia usajili, imagine.
Kuingia kwenye soko la ushindani Afrika ni labda Simba na Yanga zimilikiwe na Mtu binafsi k**a Sundowns ama Mazembe lakini kwa mfumo wa Wanachama ni lazima uwe imara k**a Al Ahly na Zamalek, ambapo hapa kwetu ni k**a bado elimu haijafika vizuri, hatujaelewa na bado hatutaki kuelewa.
GSM na MO hawana cha kulaumiwa, imagine suala la Wanachama, Yanga waliochukua kadi na kulipia ada zao za Wanachama kwa taarifa nizonazo hawafiki 25,000 nchi nzima jaribu tu kufikiria Al Ahly mtoto mdogo analipa ada 105,000 kwa mwaka, huyu unaenda kushindana nae vipi? Hapo Simba wangapi wana kadi za Mashabiki?
Matajiri wanabeba mzigo mkubwa na ni k**a Mashabiki wameziacha timu mgongoni mwao, wapo pembeni wanasubiri Kariakoo Giants waishi k**a Giants wa Afrika, hiyo ni ngumu bila Mashabiki kubadilika basi timu zitaishia kugombania wachezaji wa Ligi Kuu, watapishana kubeba Ligi Kuu na watakuwa na vikosi vya pili ambavyo vitashindwa hata kubeba Mapinduzi Cup.
Wachezaji wakubwa na wa maana wapo, wachezaji wenye thamani wapo ila pesa yote anatoa nani? Upande wa Mashabiki na wanachama wana support gani? Zaidi ya kusubiri vipaza sauti ya waandishi kuwakosoa Matajiri mambo yasipoenda sawa.
Yaani tununue pikipiki kutoka India halafu tuliite Mercedes Benz??___
[ ]