16/03/2026
Party 2/2
K**a mtu mwenye pesa nyingi akikusaidia, moja ya njia rahisi ya kurudisha fadhila huwa kumpa feedback.
Mtu akitoa msaada, huwa anataka kujua msaada wake umeleta matokeo gani. Feedback inaonesha kuwa uliheshimu kile alichokifanya na uliutumia msaada ule kwa maana iliyokusudiwa.
Feedback nzuri huwa na vitu vitatu.
• Eleza msaada aliokupa.
• Onesha matokeo yaliyopatikana.
• Shukuru kwa mchango wake.
Mfano.
Alikusaidia mtaji wa biashara. Baada ya muda mrudie na umwambie biashara imeanza, unauza kiasi gani, na changamoto zipi unakutana nazo. Hiyo taarifa ina thamani kubwa kuliko hata shukrani ya maneno pekee.
Watu wenye uwezo wa kusaidia hupokea maombi mengi kila siku. Wengi wanaopokea msaada hupotea bila kutoa mrejesho. Hali hii huwafanya wasijue k**a msaada wao ulienda sehemu sahihi.
Ukipata msaada na ukatoa feedback.
• Unaonesha uwajibikaji.
• Unajenga uaminifu.
• Unafungua mlango wa msaada mwingine siku zijazo.
Mara nyingi msaada mkubwa haukatiki kwa sababu mtu hana uwezo. Hukatikaga kwa sababu wale waliopata msaada wa mwanzo hawakurudi kutoa mrejesho.
Feedback ni ishara ya heshima. Ni ishara ya shukrani. Ni ishara ya uaminifu.