Waleed Information & Communication skills

Waleed  Information & Communication skills MISEMO

  Youtube ilianzishwa na jamaa watatu ambao walikuwa waajiriwa wa Paypal, Chad Hurley, Steve Chen na Jawed Karim mwaka 2...
26/04/2020



Youtube ilianzishwa na jamaa watatu ambao walikuwa waajiriwa wa Paypal, Chad Hurley, Steve Chen na Jawed Karim mwaka 2005, na ikaanza kuwa mtandaoni rasmi Jumatatu ya February 14, 2005, saa tatu na dakika 12 usiku.

Makao makuu yake yapo huko San bruno, California nchini marekani ambayo kwa sasa inamilikiwa na Google ambayo ilinunuliwa kutoka kwa hao jamaa November ya mwaka 2006 kwa kiasi cha dola billion 1.65.

Youtube ni website ambayo inaruhusu watumiaji wake kuweka na kuangalia video mbalimbali, kutoa maoni naku-subscribe account za watumiaji wengine.

Mpaka kufikia mwaka 2019 youtube iliingizia Google dola billion 15.

Pichani hao ndio waanzilishi wa YouTube.

JE ACCOUNT ZAKO ZA MITANDAO YAKIJAMII NA NYINGINEZO HUWA UNAZIWEKEA ULINZI WAKUTOSHA?Kila mtu huwa anajiuliza nawezaje k...
09/02/2020

JE ACCOUNT ZAKO ZA MITANDAO YAKIJAMII NA NYINGINEZO HUWA UNAZIWEKEA ULINZI WAKUTOSHA?

Kila mtu huwa anajiuliza nawezaje kuweka ulinzi kwenye account zangu k**a instagram na nyinginezo?.......

kimsingi vyote hivyo vinakuwa controlled na e-mail yako, k**a unatumia android automatic utatumia Gmail account na mtu akiweza kupata hiyo email yako anaweza aka-access vitu vyako vya private k**a meseji picha na vingine.....

Ndio maana unasikia mara mtu amehack (amedukua) account yako ya insta, facebook or whatever.....basi ujue alipata email or password yako na anaweza kucontrol kila sehemu ambapo umelink hiyo email though sasa hivi kuna technique nyingi sana zaku-hack naku-access account mbali mbali watu wanahack mpaka data za siri za serikali ya marekani k**a ushawahi kusoma au kusikia ile scandal ya Edward Joseph snowden ambayo nilishawahi kuipost before....

Hakuna kitu chakuzingatia na cha msingi k**a security (ulinzi) unapotumia simu au computer au vitu vinavyofanana na hivyo.......

mfano iphone wanakitu kinaitwa advertising ukiwa umekiruhusu (allow) kwenye simu yako utakuta ukiingia kwenye site mbali mbali unaanza kuona matangazo mbali mbali ambayo yanaendana na vitu unavyopenda sababu washajua vitu ambavyo unapenda sana kuvifatilia........

Dunia sasaiv imepiga sana hatua kutokana na utandawazi so unapotumia hivi vifaa vya teknolojia ya computer zingatia sana kitu kinachoitwa SECURITY (ULINZI)..


Jitahidi sana kuwa unabadilisha password ya account zako kila baada ya muda fulani pia usijaribu kutumia password moja kwenye kila account....

Mfano wengine wanatabia yakutumia password moja kwenye Facebook, instagram Twitter, Gmail, Yahoo n.k hii yote nikuepuka kusahau lakini ni hatari sana kwa usalama wa account zako....

Cha mwisho jitahidi sana unapotengeneza password tengeneza password ngumu kuing'amua epuka kutumia namba tupu au maneno tu, jitahid kuchanganya maneno, namba na characters nyengine k**a #$%@! Itakusaidia sana...

Be big than your biggest fear, adios amigo ciao 👊

Hiki kifaa ukikiweka kwenye meno yako kinaweza kutambua aina ya kitu ulichokula na kutuma taarifa kwenye simu yako.........
30/01/2020

Hiki kifaa ukikiweka kwenye meno yako kinaweza kutambua aina ya kitu ulichokula na kutuma taarifa kwenye simu yako......

kifaa hicho ambacho kipo k**a stika upande mmoja kimeundwa na dhahabu na upande wa ndani kimeundwa na material ya bioresponsive ambayo ipo vizuri sana katika kutambua vitu vinavyoingia mdomoni......

watengenezaji wa kifaa hicho wanaamini kwamba matumizi yakifaa hicho yatasaidia watu wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kisukari ,shinikizo la damu kuweza kutambua kiasi cha vyakula vya aina mbali mbali wanavyotumia.....

Huyu jamaa anaitwa Jan Koum ndio mgunduzi wa mtandao wa kijamii wa whatsapp ambao ulianza kutumika rasmi mwaka 2009, ni ...
26/04/2018

Huyu jamaa anaitwa Jan Koum ndio mgunduzi wa mtandao wa kijamii wa whatsapp ambao ulianza kutumika rasmi mwaka 2009, ni mmarekan aliyezaliwa katika jiji la Kiev nchini Ukraine lakini asili yake ni myahudi(Jewish) wa huko Israel.

Kasomea mambo ya computer programming, pia alishawahi kufanya kazi yahoo baadaye akaacha pia kabla hajagundua hii application ya whatsapp alishawahi kwenda kuomba kazi facebook lakin alikataliwa kwakuwa hakuwa na vigezo walivyotaka lakin baadae alipogundua hii program hao hao facebook walimfata nakumuomba awauzie hii program kwa dola za kimarekan billion 19.3 na yeye pia wamuajiri awe k**a ni miongoni mwa wafanyakazi wa facebook.

Kwahiyo mwaka 2014 ilianza kumilikiwa rasmi na facebook ya Mark Zuckerberg, mwaka 2014 aliingia katika jarida la forbes k**a miongoni mwa wamarekani 400 matajiri duniani na alishika nafasi ya 62.

Huyu jamaa anaitwa Kevin Systrom, alikuwa anajifunza programming kila siku usiku akitoka kazini baadae akaja kutengeneza...
25/04/2018

Huyu jamaa anaitwa Kevin Systrom, alikuwa anajifunza programming kila siku usiku akitoka kazini baadae akaja kutengeneza program iitwayo Burbid ambayo ilikuwa inasaidia watu kujua mahali walipo, kushare picha n.k.

Baadae aliiuza kwa dola 500,000 na akaacha kazi aliyokuwa akiifanya.

Then akadesign program nyingine iitwayo Istagram (hii tunayojishaua nayo mitandaoni) kwakutumia mfumo ule ule wa ile program ya kwanza (Burbin) but akaiuza pia kwa dola billion 1 kwa mmiliki wa facebook mark zuckerberg,

ndio maana istagram wameilink na facebook kias kwamba unaweza ukapost picha instagram afu ukaishea facebook at the same time.

Kwahiyo istagram na facebook zinamilikiwa na mtu mmoja.

Anaitwa Edward Joseph Snowden alizaliwa mwaka 1984 huyu jamaa ni professional wa computer ambaye aliwahi kufanya kazi Ka...
04/11/2017

Anaitwa Edward Joseph Snowden alizaliwa mwaka 1984 huyu jamaa ni professional wa computer ambaye aliwahi kufanya kazi Katika Kampuni ya Dell baadae akaajiriwa na shirika la kijasusi la marekani Central Intelligence Agency (CIA) na baadae alikuja kufanya kazi National Security Agency(NSA.

Huyu jamaa amekuwa maarufu miaka ya hivi karibuni kwasababu alivujisha taarifa za siri za serikali ya marekani kitu ambacho kimemtia matatizoni mpaka sasa hivi anaishi uhamishoni nchini Urusi(Russia).

Huyu Mmarekani alikuwa akifanya kazi k**a System Administrator lakini ni mdukuzi(Hacker) hatari ambae anaweza akawasha simu yako hata k**a umeizima bila kuishika akiwa upande wa pili wa office yake, pia ana uwezoi wakumpigia mtu mwengine simu kwakutumia simu yako ikiwa mfukoni kwako!!..

Leo nimeona kidogo tuongeze kitu cha msingi kichwani kwakumfahamu huyu jamaa kwa ufupi....thnx

Sharing is caring....share na wengine wajue

Waleed techâ„¢

KAA TAYARI KUJIFUNZA JINSI YAKUTUMIA SIMU YAKO K**A MODEM KWENYE COMPUTER/LAPTOP YAKO...LIKE HII PAGE USIPITWE
27/09/2017

KAA TAYARI KUJIFUNZA JINSI YAKUTUMIA SIMU YAKO K**A MODEM KWENYE COMPUTER/LAPTOP YAKO...LIKE HII PAGE USIPITWE

27/09/2017

JE UKIWEKA BANDO HUWA APPLICATION ZAKO ZINAJI-UPDATE KABLA UJAZIRUHUSU NAKUKUMALIZIA BANDO LAKO?

FANYA YAFUATAYO ILI KUZUIA ZISIJI-UPDATE AUTOMATICALLY

Fungua google playstore then upande wa juu kulia au kushoto inategemea na setting za simu yako utaon vistari vitatu bonyeza then >>settings >> auto-upadate apps>> then chagua do not auto-update app.

Baada ya hapo utakuwa umesitisha application kuji-update zenyewe kabla hujaziruhusu.

Je, k**a umeweka kifurushi chakutosha na unataka ku-update application zako utafanyaje?

Fanya yafuatayo:-

K**a hizo hatua hapo juu ila ukishabonyeza hivyo vistari vitatu then bonyeza sehemu iliyoandikwa MY APPS & GAMES baada ya hapo utaziona application zote zinazohitajika kufanyiwa up-dates....

unaweza ukaup-date zote kwakuchagua updates all au ukaup-date moja moja kulingana na ukubwa wa bando lako kwasababu application nyingine ukiziup-date zinachukua bando kubwa.

Share na wengine wajue kisha like page hii usipitwe na post mbali mbali ambazo naziandaa ikiwemo za Computer/laptop

Till next tym

28/08/2017

JE UNAJUA SIM card NI NINI? ONGEZA UFAHAMU HAPA

Kirefu cha SIM card ni (Subscriber Identity Module) ni kifaa ambacho kinahifadhi habari mbali mbali za mtumiaji hasa kwa sisi ambavyo tunavyoielewa zaidi kwakuwa tunaitumia sana kwenye simu zetu ambayo inajulikana k**a line ya simu.

Hiki ni kifaa ambacho kimebadilisha ulimwengu wa mawasiliano tangu kilivyotengenezwa mwaka 1991 na bwana anayejulikana k**a Giesecke ambaye mara ya kwanza alitengeneza SIM card 300 akaziuza.

Katika hiyo miaka ya tisini ambapo simu za mkononi zilikuwa kubwa SIM card zilikuwa na saizi sawa na credit card hizi tunazotumia kufanya miamala mbali mbali katika mabenki.

KAZI YA SIM card

Kazi kubwa ya hizi SIM card ni kuhifadhi habari mbali mbali za mtumiaji k**a:-

-Kuhifadhi namba za mawasiliano(Contact list)

-Namba binafsi za ulinzi(Personal security keys) k**a PIN na PUK

-Meseji mbali mbali za simu(text messages)

-Data za umiliki wa mtandao(Network authorization data)

Hizi SIM card zipo za ukubwa (size) mbali mbali k**a:-

Size kubwa (Full size) 1FF Hizi hutumika kwenye kadi za benki k**a smart cards na nyinginezo

Size ya kati (Mini size) 2FF hizi ambazo tunatumia katika simu zetu

Size ndogo (Micro size) 3FF

Size ndogo kabisa (Nano) 4FF

LIKE PAGE KISHA SHARE

24/08/2017

JE HUPENDI BAADHI YA RAFIKI ZAKO WANAPOKU-TAG PICHA FACEBOOK?

JIFUNZE JINSI YAKUZUIA MTU ASIKU-TAG HAPA...

Kuna baadhi watu wanapenda sana ku-tag picha rafiki zao facebook japo kuna wengine huwa hawapendi kitu k**a hiki kwasababu zao mbali mbali, labda kuna wengine huwa-tag picha ambazo hazina maadili n.k

FATA HATUA ZIFUATAZO ILI KUZUIA MTU ASIKU-TAG

1. Fungua app yako ya facebook then upande wa juu kulia utaona vistari vitatu bofya hapo

2. Baada ya hapo chagua sehemu iliyoandikwa >>Account setting

3. Then chagua sehemu iliyoandikwa >> Timeline and tagging

4. Halafu utaona kuna maandishi yalioandikwa >> who can post on your timeline bofya hapo.

5. Pakifunguka utaona kuna machaguo mawili:-

Friends
Only me

Wewe chagua only me mpak uone ile alama ya tiki(√) imehamia kwenye hilo neno Only me basi hapo tayari

PIA UNAWEZA USIZUIE WATU WAKU-TAG ILA PINDI ATAKAPOKU-TAG HAIWEZI KUTOKEA KWENYE WALL YAKO MPAKA UIRUHUSU LAKIN FACEBOOK WATAKUJULISHA KWAMBA KUNA MTU AMEKU-TAG THEN WEWE UTACHAGUA KUIRUHUSU AU KUTOKUIRUHUSU ITOKEE KWENYE TIMELINE YAKO

K**A UNATAKA HII
Fuata hatua k**a hizo hapo juu lakini ukifika kwenye hayo maandishi yalioandikwa >>who can post on your timeline kwa chini yake kuna maandishi mengine utayaona yameandikwa>> Review posts friends tag you in before they appear on your timeline.....basi bofya hii option

>>Then utaona kuna neno limeandikwa>>Timeline

>>Mbele ya hilo neno kuna otion mbili za ON na OFF wewe weka ON baada hapo utakuwa umekamilisha

LIKE PAGE HII USIPITWE NA MAMBO MENGI ZAIDI, SHARE KWA WENGINE PIA ILI NAO WAPATE KUJUA

>>>>>>>>>>>Asanten

19/08/2017

Post iliyopita nilielezea kidogo mambo yanayopelekea betri ya simu yako isiwe na uhai mrefu nakupoteza uwezo wake wakuhifadhi chaji kwa muda mrefu

Sasa leo nitaendelea kuelezea kwa undani zaidi k**a kukazia nakuongezea mambo baadhi

TWENDE PAMOJA

1. Epuka kuchaji mara kwa mara simu yako kwakutumia kihifadhi chaji(Power bank)

>>Power bank huhifadhi chaji k**a betri la simu lilivyo hivyo kitendo chakuchaji betri lingine husababisha maambukizi ya mtiririko wa chaji hivyo kufanya betri kupoteza nguvu yakuhifadhi chaji kadri unavyozidi kutumia mara kwa mara.

2. Epuka kutumia Applications zenye matangazo mengi

>>Kwenye majaribio mbali mbali yaliyofanywa na wataalam wa mitandao yamebaini kuwa apps zenye matangazo mengi huchukua karibia 30% ya chaji pindi unapozitumia..
>> Kwahiyo unashauriwa kupunguza kutumia app hizi au kuzitoa kabisa

3. Tumia charger sahihi kwa simu yako

>>Kila simu ukisoma kwa nyuma kuna maelezo yameandikwa kuwa usitumie charger nyingine mbali na ile uliyopewa na simu
>>Charger huwa na voltage( Kiasi cha umeme kipitacho kwenye waya) yake inayopita kuchaji simu na hii hutofautiana kutokana na ukubwa na aina ya simu,

Kwahiyo k**a simu yako inapitisha mfano voltage 0.05 naukatumia charger inayopitisha 0.5 lazima uharibu betri yako..

Hivyo ni bora ukajua simu yako inapitisha kiasi gani cha umeme kabla yakutumia charger nyingine.

4.Epuka kuchaji simu na kuiweka katika mazingira ya joto kali

>>Simu nyingine hususani zile za kisasa hutakiwi kuziweka kwenye mazingira ya joto kali zaidi ya 50% kwakufanya hivyo kutafanya betri ya simu yako kupungua nguvu...epuka kuchaji simu juani

5. Chaji simu yako pale inapofikia 16%-10%

>> Wataalam wa maswala ya kielectronic wanasema chaji simu yako pale tu inapoanza kutoa mlio wakuashiria betri yako inahitaji kuchajiwa, usisubiri mpaka simu yako izime kabisa kwani kwakufanya hivyo kutaathiri ions ambazo huhifadhi chaji na kwa muda mfupi utaona simu yako ikipoteza uwezo wake wakuhifadhi chaji kabisa.

6. Kutokuchaji simu kwa ufasaha
>> Hiki ni kitendo cha kutoa simu kwenye chaji kabla haijajaa ni kosa kubwa, subiri mpak simu yako ijae chaji kabisa labda itokee dharura.

7. Epuka kuchaji simu ikiwa hewani

>>Zima simu yako au iweke katika flight mode ni vizuri zaidi kwakuwa simu inajaa chaji vizuri ikiwa imewaka lakin haitumiki.

>>Pia ni vizuri zaidi simu yako kuizima au kuiweka katika flight mode kwakuwa huchukua muda mfupi pia kujaa..

Asanten share na wenzio wajue

18/08/2017

BAADHI YA VITU VINAVYOCHANGIA BATTERY ZA SIMU KUFA KWA HARAKA

Ukiachana na hizi battery za kichina, unaweza ukaenda dukani ukanunua battery nzuri tu original lakini ukaitumia siku si nyingi ikaanza kupoteza uwezo wake wakuhifadhi chaji kwa muda mrefu..

Cheki na hizi sababu huwenda ukawa unayafanyaga haya nakusababisha battery lako kupoteza uwezo wake wakuhifadhi chaji:-

1. Kutumia simu wakati unaichaji

Wengi huwa wanalifanya sana hili, kitu ambacho kinapelekea battery yako kupata joto sana na pia ni hatari hata kwa simu yako..si vizuri kutumia simu wakati unaichaji iache kwanza ijae

2. Kutumia chaji ambayo si sahihi kwa simu yako ..Tumia chaji ambayo ni sahihi kwa simu yako sio wewe unatumia Samsung unachajia charger ya Tecno...k**a una simu ya tecno tumia charger ya tecno k**a samsung tumia charger yake n.k.

3.Kuchaji kwakutumia USB cable

Hili hasa ni kwa wale ambao hutumia computer au laptop kuchajia simu zao ambao huondoa kile kichwa cha charger nakutumia cable peke yake kuchomeka kwenye zile USB port za computer...tafuta tu switch utumie cable na kichwa chake kuchajia simple like that

4. Kuendelea kuchaji simu hata k**a imejaa

K**a simu imeshajaa iondoe kwenye charger yake tumia kawaida unauwa battery yako!!!

Ushauri:

Ni vizuri zaidi wakati unachaji simu ukaiacha ijae kabisa si vizuri kuchaji halafu kabla haijajaa ukaichomoa nakuanza kuitumia

Pia si vizuri kuendelea kutumia simu ambayo chaji yake ipo chini ya 16%-10% ni vizuri ukaacha kutumia nakuiweka kwenye chaji kwa afya ya battery yako

Post itakayofuata nitazielezea kwa undani zaidi kwa leo ngoja niishie hapa

Asanten

Address

Waleedmohameed009@gmail. Com
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 06:00 - 05:00
Tuesday 06:00 - 05:00
Wednesday 06:00 - 05:00
Thursday 06:00 - 05:00
Friday 06:00 - 05:00
Saturday 06:00 - 05:00
Sunday 06:00 - 05:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Waleed Information & Communication skills posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share