14/06/2025
Hujambo......Kuna hii tabia kwamba una mume wako au hata mpenzi wako tu ambaye bado hamjaoana, huyu mwanaume anakupiga matukio mazito alafu hataki kuomba msamaha, yani kuna mwanaume umemfumania na mwanamke mwingine, iwe live au kwenye simu kuna viashilia vinaonyesha ni wapenzi, unapojaribu kumuuliza kwanini unafanya hivi? anakujia juu kwamba unamchunguza.
Kuna aina ya mwanaume ambaye anakukosea ukionyesha kuchukizwa na kosa lake hakuombi msamaha ananuna wiki nzima na anataka wewe ndiye umuombe msamaha ili muendelee kuzungumza ndani. Please 🙏 usifanye hivyo, kuomba msamaha sio ujinga lakini k**a mwanaume wako amekukosea alafu hajutii kosa lake na anakugeuzia kibao kutaka wewe ndiye umuombe msamaha usikubali.
Kwa kufanya hivyo hauponyi ndoa yako unaidumaza na unajitia kwenye kifungo wewe mwenyewe, kwasababu hapo sasa mwanaume atakuwa haogopi kukukosea kwasababu ameshaelewa kwamba anakumudu hata akukosee vipi huwezi kufanya chochote. Mara moja moja mwanamke onyesha msimamo, kuna muda mwanaume anakufokea ukimuona amekaza uso unasema huyu kacharuka kwelikweli kumbe moyoni anakuogopa.
Usiwe mnyonge sana unapoona kuna mahali unaonewa simama kwenye nafasi yako, iteteee nafasi yako k**a mke, unyonge ukizidi unalemaza mahusiano, na kwakufanya hivyo haumzarau mwanaume isipokuwa upo kwenye nafasi yako. Haijakaa sawa mwanaume anakukosea alafu hatambui makosa yake, huyu hata mapenzi ya kweli anakuwa hana.
Wakati mwingine mnawalemaza waume zenu wenyewe kwasababu kuna wakati akikukosea akanuna wewe unaanza "basi nisamehe mimi mume wangu hata k**a sina kosa" hii sio nzuri, inaua mahusiano inaondoa furaha inaleta karaha. Kuna sheria na kanuni za ndoa, zifuateee, kuwa makini unapokuwa kwenye ndoa yako, ndoa inaanza vizuri baada ya muda inakuwa mbaya, wengi wenu mnakimbilia kuwalaumu wanaume wakati chanzo ni nyie mlivyowapokea hapa mwanzo wa ndoa, mwisho wa siku wanachukulia mazoea wanabadilika.
KARIBU UZUNGUMZE NAMI 👉 0629596654