Muona Mbali Kaona

Muona Mbali Kaona Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Muona Mbali Kaona, Information Technology Company, Bwawani Street, Dar es Salaam.

Matukio mbalimbali kwenye hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Maafisa na Wakaguzi Wasaidizi wa Jeshi la Polisi, kozi namba 1...
28/05/2026

Matukio mbalimbali kwenye hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Maafisa na Wakaguzi Wasaidizi wa Jeshi la Polisi, kozi namba 1 ya mwaka 2025/2026, Kurasini Jijini Dar es Salaam, tarehe 28 Mei, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitoa vyeti kwa Wahitimu wal...
28/05/2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitoa vyeti kwa Wahitimu waliofanya vizuri kwenye Mafunzo ya Maafisa na Wakaguzi Wasaidizi wa Polisi, kozi namba 1 ya mwaka 2025/2026 katika Chuo cha Taaluma ya Polisi, Kurasini Jijini Dar es Salaam, tarehe 28 Mei, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride lililoandali...
28/05/2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride lililoandaliwa na Jeshi la Polisi kabla ya kuhitimisha Mafunzo ya Maafisa na Wakaguzi Wasaidizi wa Jeshi hilo, Kurasini Jijini Dar es Salaam, tarehe 28 Mei, 2026. .tanzania .hajiomar @ .hmwinyi .tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati wimbo ...
28/05/2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati wimbo wa Taifa ukiimbwa kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Polisi, Kurasini Jijini Dar es Salaam, tarehe 28 Mei, 2026.

Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kupitia akaunti zetu za Instagram: ikulu_mawasiliano, Facebook: Ikulu Tanzania Faceb...
28/05/2026

Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kupitia akaunti zetu za Instagram: ikulu_mawasiliano, Facebook: Ikulu Tanzania Facebook fanpage: Ikulu Mawasiliano, Twitter: ikulu_Tanzania Youtube Channel:
Ikulu Tanzania na Tovuti: www.ikulu.go.tz


 @    .hmwinyi           .tanzania
27/05/2026

@ .hmwinyi .tanzania

DKT. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE▪️Wakubaliana kuimarisha masuala ya kilimo, nishati na usalama WAZ...
27/05/2026

DKT. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

▪️Wakubaliana kuimarisha masuala ya kilimo, nishati na usalama

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amekutana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Congo, Anatole Collinet Makosso na kujadiliana naye masuala ya kidiplomasia ikiwemo usalama, mazingira, kilimo na nishati kwenye kikao kilichofanyika ofisini kwa mwenyeji wake, Boulevard Alfred Raoul, Brazzaville, jijini Brazzaville.

Akizungumza na mwenyeji wake leo (Jumatano, Mei 27, 2026) Dkt. Mwigulu amesema mbali na kupata fursa ya kushirki mkutano wa mwaka wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), ziara yake nchini Congo ni ya kukuza mahusiano baina ya nchi hizo mbili.

“Ujio wetu nchini Congo Brazzaville, umelenga kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia lakini pia kuhimiza haja ya nchi zetu kukuza ushirikiano wa kikanda, kutunza utulivu, amani na maendeleo ya bara la Afrika.”

Alimwelezea mikakati ambayo Dkt. Samia ameiweka katika kukuza kilimo kupitia njia ya umwagiliaji, kukuza uchumi kupitia sekta ya utalii na suala zima la uhifadhi wa mazingira.

Waziri Mkuu pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Congo, Denis Sassou-Nguesso kwa kumualika Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kushiriki mkutano huo ambao ilimpendeza kumtuma yeye amuwakilishe.

Ametumia fursa hiyo kufikisha ujumbe wa Dkt. Rais Samia Suluhu Hassan wa kuiomba nchi ya Congo imuunge mkono mgombea wa Tanzania kwenye nafasi ya Jaji wa Mahakama ya Kimataifa (ICC), Dkt. Deo John Nangela ambaye uchaguzi wake umepangwa kufanyika Desemba, mwaka huu jijini New York, Marekani.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Congo alimshukuru Dkt. Mwigulu kwa kushiriki mkutano huo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye alisema anatambua kwamba ana majukumu mengine ya kitaifa.

Alisema nchi hiyo ina mengi ya kujifunza kutoka Tanzania hasa kwenye sekta ya nishati. “Ninajua kwamba hakuna maendeleo bila uwepo wa umeme au nishati. Na nchi ya Tanzania iliitisha mkutano mkubwa wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati ujulikanao ‘misheni 300’ ambao unalenga kuhakikisha wananchi milioni 300 barani Afrika wanapata umeme ifikapo mwaka 2030. Tunapaswa tuungane kutafuta fedha za kuendeleza mradi huu,” alisisitiza.

WAZIRI MKUU AKUTANA NA PROF. JANABI BRAZZAVILLEWAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Sh...
27/05/2026

WAZIRI MKUU AKUTANA NA PROF. JANABI BRAZZAVILLE

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika (WHO AFRO), Profesa Mohamed Janabi ambapo walijadili masuala mbalimbali ya maendeleo, hususan ushirikiano katika sekta ya afya barani Afrika.

Pia, Dkt. Mwigulu alikutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Balozi Stephen Mbundi pamoja na Katibu Mkuu wa Jukwaa la Mabunge ya Ukanda wa Maziwa Makuu Afrika (FP-ICGLR), Balozi Dkt. Deo Mwapinga.

Mazungumzo hayo yamefanyika kando ya Mkutano wa 61 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), unaoendelea jijini Brazzaville, Jamhuri ya Kongo leo Jumatano Mei 27, 2026.

Address

Bwawani Street
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Muona Mbali Kaona posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share