16/04/2026
Mfumo wa Ulinzi ujulikanao k**a IRON DOME.
Iron dome ni technolojia ya Ulinzi wa anga ambayo inatumiwa na jeshi la Israel kwaajili ya kuzuia makombora ya masafa mafupi.
Inaelezwa kuwa mfumo wa Iron dome unazuia makombora ya umbali wa kilomita 4 mpaka 70 kwa ufanisi mkubwa.๐
Sehemu ya mfumo huu (Iron dome) unajumuisha rada ya kugundua na kufuatia, mfumo wa kudhibiti na kuangalia k**a kombora litaangukia eneo la makazi ya watu au laa.
Mfumo huu unaweza kufanya kazi katika mazingira yeyote ya hali ya hewa, iwe usiku au mchana kwa ufanisi mkubwa, ikiwemo wakati wa mvua, ukungu au vumbi. Mfumo huu hulinda eneo hadi kilomita 150 kwa bettri moja.๐
Bettri moja ya mfumo wa Iron dome inajumuisha mfumo kamili ambao huwa na makombora 60 mpaka 80 na kuweza kulinda eneo la kilomita 150.
Mfumo wa Iron dome ulianza kufanya kazi mwaka 2011, na Israel inapata ufadhili mkubwa toka serikali ya marekani katika uzalishaji na uendelezaji (unagharimu pesa nyingi).๐ฅบ
Mfumo huu wa Iron dome unaendeshwa kwa gharama kubwa sana, kwa maana ya Pesa, ambapo bettri moja ya Iron dome inagharimu dollar za kimarekani million 100, na hiyo bettri moja inaendesha makombora 60 mpaka 80 na gaharama ya kombora moja ni dollar za kimarekani elfu 40000 mpaka dollar laki 1. (Kwa nchi zinazoendelea kumiliki mfumo huu ni kujitafutia umaskini)๐
Iron dome unaambiwa inaufanisi mkubwa zaidi wa kudungua makombora, ambapo ufanisi wake unafikia hadi asilimia 90% katika utendaji kazi wake, pia unatoa uelekea wa kombora kabla halijatua chini. Mfano k**a kombora litaangukia eneo ambalo halina makazi ya watu au eneo lenye umuhimu basi mfumo hautawajibika kudungua kombora hilo.๐
NB: Israel๐ฎ๐ฑ inamifumo mingi ya Ulinzi wa anga k**a vile Iron dome, Iron beam (Mionzi), THAAD(USA), Arrow 2 na Arrow 3, David's sling.
Ila Iran nao wanakitu wasipuuzwe kwa mifumo hii bado kombora linapita balaa!!๐๐
Follow ukurasa wetu