23/08/2016
Ni wengi wanaoutumia na kuufahamu mchaichai k**a kiungo cha chakula jikoni na wengine hutumia k**a dawa ya mbu. Lakini, je unafahamu kuwa majani haya yana faida kubwa kiafya . Mafuta ya mchachai hutumika katika viwanda vinavyotengeneza pafyumu na sabuni.
Tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa mchaichai una vichocheo muhimu vinavyoweza kupambana na athari kadha wa kadha tumboni, kwenye mkojo na hata kwenye vidonda.
Watu wengine huamini kuwa mchaichai unaweza kutibu baadhi ya maradhi k**a vile homa ya matumbo, matatizo ya ngozi, madhara yanayotokana na ulaji wa chakula chenye uchafu na pia hutibu maradhi ya kichwa na hata misuli. Mchaichai pia unatajwa kuwa kinywaji kinachoweza kupunguza joto. Chai ya mchaichai inasaidia kupunguza joto kwa mgonjwa wa homa. Faida nyingine za mchaichai kiafya ni pamoja na Kinga dhidi ya saratani.